Search This Blog

Monday, March 11, 2013

KOCHA WA YANGA: WASHAMBULIAJI WANGU BUTU - DAKIKA 270 WAMECHEZA BILA GOLI


KOCHA wa Yanga, Ernie Brandts amekiri kazi imewashinda washambuliaji wake kwani dakika 270 wamemaliza bila kupachika wavuni bao lolote.
 

Washambuliaji hao Jerry Tegete, Didier Kavumbagu, Said Bahanuzi na Hamis Kiiza wameshindwa kufunga bao hata moja katika mechi tatu mfululizo jambo ambalo linawafanya viungo wa timu hiyo kuwaokoa kwa kufunga katika mechi hizo.
 

Katika mechi tatu zilizopita, Yanga ikicheza na Azam FC, Kagera Sugar na Toto African, imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0. Mbali na ushindi huo, mabao yote matatu ya Yanga y katika mechi hizo yamefungwa na viungo, Haruna Niyonzima aliyefunga mawili katika mechi dhidi ya Azam na Kagera na Nizar Khalfan aliyefunga moja dhidi ya Toto.
 

Washambuliaji, Jerry Tegete, Hamis Kiiza na Didier Kavumbagu wamekosa umakini na kupoteza nafasi nyingi za wazi kupachika mabao jambo ambalo linamkwaza kocha wao.
 

Brandts ameshangazwa na hali hiyo na kushindwa kuamini kile anachokiona na kudai kuwa hivi sasa amekuwa akiwategemea viungo ndio wafunge mabao kwani washambuliaji kazi imewashinda. Mholanzi huyo alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa haelewi kitu kilichowapata mafowadi wake, lakini amesisitiza kuandaa programu ambayo anaamini itamaliza tatizo hilo.
 

"Sielewi kitu gani ambacho kimewakumba vijana wangu kwa siku za hivi karibuni." alisema kocha huyo aliyevaa viatu vya Mbelgiji, Tom Saintfiet aliyetupiwa virago Septemba mwaka jana.
Brandts alisema kubwa ambalo ameligundua kwa wafungaji wake ni kukosa umakini hasa wamapolifia lango.
 

"Kila mara nimekuwa nikiwaeleza kuweka utulivu wanapolikaribia lango,lakini bado tatizo hilo linajirudia."
 

Alisema;"Kwa sasa tumekuwa tukiwategemea viungo wafunge. Tumeshinda mechi tatu zilizopita dhidi ya Azam, Kagera na Toto, lakini katika mazingira magumu."

___

No comments:

Post a Comment