Search This Blog

Friday, March 8, 2013

IMEFAHAMIKA ALIYEMUWEKEA MALINZI PINGAMIZI UCHAGUZI WA TFF AMESOMA NA NYAMLANI NA MWENYEKITI WA KAMATI RUFAA ALIYEMUENGUA MALINZI

MGOMBEA nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani, Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya uchaguzi wa shirikisho hilo, Idd Mtiginjola pamoja na Agape Fue, wote ni wahitimu wa sheria kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa, imefahamika.
Fue alitikisa duru za soka hapa nchini baada ya kumwekea pingamizi mgombea wa nafasi ya urais wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi. Hata hivyo alipoulizwa kuhusu hilo, Mtiginjola alicheka kabla ya kukubali na kusema: "Kwani kuna tatizo gani, mbona hamniulizi kuhusu Wambura (Michael) ambaye niliwahi kusoma naye Mzumbe?"
Alisema vyuo vikuu nchini vinajulikana na kwamba ni ujinga na upuuzi kuzungumzia suala la yeye kusoma na mtu kwani mwenye akili timamu anajadili hoja na si mtu.
"Ni upuuzi kujadili watu, tujadili hoja iliyopo mezani, ukishaanza na hoja za aina hiyo hoja itakayofuata itakuwa ni ya ukabila, utahoji mbona huyu na huyu Wahaya, kitaaluma hiyo si sahihi,'' alisema.
Pamoja na kuweka pingamizi hilo Fue, aliyepata shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa mwaka 2005, alishindwa kutokea siku aliyotakiwa kuthibitisha pingamizi lake kwa Malinzi mbele ya kamati uchaguzi.
Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa TFF, mkata rufaa akishindwa kutokea basi pingamizi lake huwa batili.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa, Mtiginjola ambaye alisoma pamoja na Fue katika Chuo cha Tumaini na kumaliza naye mwaka 2005 aliamua kutumia rufaa hiyo kumwengua Malinzi kwenye kinyang'anyiro.
Kuenguliwa kwa Malinzi kulimfanya Athuman Nyamlani, ambaye pia alisoma shahada ya sheria Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa, lakini akimaliza kabla ya Fue na Mtiginjolo kuwa mgombea pekee kwenye nafasi ya urais kitendo kilichozua mzozo mkubwa kutoka kwa wadau wa soka nchini.
Uchaguzi wa TFF ulipangwa kufanyika Februari 24 mwaka huu, lakini ukaahirishwa kutokana na Fifa kuingilia kati kabla ya Serikali kuifuata katiba mpya ya TFF iliyokuwa itumike kwenye uchaguzi huo.a

6 comments:

  1. HUO NI MPANGO MAALUM WALIOUPANGA UONGOZI MZIMA WA TFF WANAUJUA, NDIO MAANA NASISITIZA HAWA WATU WOTE WALIOHUSIKA NA MCHAKATO HUU WANATAKIWA KUHOJIWA NA TAASISI ZINAZOHUSIKA NA MAMBO YA UCHUNGUZI NIKIWA NA MAANA:-
    1. TAKUKURU
    2. USALAMA WA TAIFA- KUNA KITU KINAFICHWA.
    3. CAG- WACHUNGUZE MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA
    4. UMMA WA WATANZANIA UJULISHWE FUE NINA, NA ANAFANYA NINI HIVI SASA NA KABLA YA NAFASI ALIYONAYO SASA
    MIMI BINAFSI, SIJUWI NYIE WENZANGU, HAWA WATU WOTE PAMOJA NA BWANA FUE, WAKIWA NI WANASHERIA NA WAMEFAULU VIZURI KWA VIWANGO VYA KITANZANIA, BILA KUTUMIA "DESA", WALITAFASIRI VIPI HIYO SHERIA WALIOISIMAMIA KUENGUA WAGOMBEA HUKU WAKIJUA NI TARATIBU ZINASEMAJE KWA MTU ALIEWEKA PNGAMIZI ANATAKIWA AFANYE NINI ILI IWEZE KUSHUGHULIKIWA, PILI NA HASA BWANA MTINGIJOLA KWANI HAKUFUATA SHERIA INAVYOSEMA KWA UPANDE HUO, KWAMBA PINGAMIZI ILI LICHUKULIWE KWELI LINATAKIWA VIPI, AU ALITUMIA TAFASIRI ILIYOMPA NGUVU KUFANYA ALIYOFANYA. TENGA KAMA RAIS NA NDIYE ALIWATEUA, SIDHANI KAMA SHERIA INASEMA HANA NGUVU YA KUTENGUA, JE HATA KUTOA USHAURI WA KISHERIA WAKATI AKIJUA SHERIA IMEPINDISHWA. KWANINI ASIVUNJE KAMATI NA KUUNDA NYINGINE ? INAINGIA AKILINI KWELI ?
    HAWA WATU KWA PAMOJA WANAJUA WANACHOKIFANYA KWA MAKUSUDI KABISA NA SIO KWA LENGO LA KUJENGA SOKA KAMA ANAVYOPIGIA KELELE, BALI KWA MANUFAA YAO

    ReplyDelete
  2. Hiyo sio hoja msingi.
    Sasa na Jk alimchagua Pinda kisa kasoma nae UDSM. Vipi kuhusu karibu zaidi ya nusu baraza kuwa wamesoma UDSM.
    Tuache majungu jamani vyuo vyenyewe vichache hapa mjini kila mtu anasoma humo humo tuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. hayo sio majungu, kumbuka haya yote yamekuja sababu ni wao wenyewe laiti wasinge fanya upuuzi huu nani angejua,hapo hakuna majungu wewe au mimi hata wao HATUJUANI,KIPATO CHAKO,CHANGU NA CHAO HAVIHUSIANI WALA HAWANIPUNGUZII ila wanashindwaje KUSIMAMIA HAKI AMBAYO HAITAJI DEGREE, sheria iko wazi wakaombwa kama binadamu wajirekebishe HAWATAKI sasa utamlaumu, USIKIMBILIE KUSEMA MAJUNGU KWA KASHINDWA KUDADAVUA MAMBO, KESHO WANASHIKA UONGOZI MWINGINE UNAFiKIRI WATAFANYA nini, NDIO MWANZO WA MIKATABA MIBOVU, NDIO MAANA NASEMA HAWA NAO NI MAFISADI.

      Delete
  3. HUO NI MPANGO MAALUM WALIOUPANGA UONGOZI MZIMA WA TFF WANAUJUA, NDIO MAANA NASISITIZA HAWA WATU WOTE WALIOHUSIKA NA MCHAKATO HUU WANATAKIWA KUHOJIWA NA TAASISI ZINAZOHUSIKA NA MAMBO YA UCHUNGUZI NIKIWA NA MAANA:-
    1. TAKUKURU
    2. USALAMA WA TAIFA- KUNA KITU KINAFICHWA.
    3. CAG- WACHUNGUZE MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA
    4. UMMA WA WATANZANIA UJULISHWE FUE NINA, NA ANAFANYA NINI HIVI SASA NA KABLA YA NAFASI ALIYONAYO SASA
    MIMI BINAFSI, SIJUWI NYIE WENZANGU, HAWA WATU WOTE PAMOJA NA BWANA FUE, WAKIWA NI WANASHERIA NA WAMEFAULU VIZURI KWA VIWANGO VYA KITANZANIA, BILA KUTUMIA "DESA", WALITAFASIRI VIPI HIYO SHERIA WALIOISIMAMIA KUENGUA WAGOMBEA HUKU WAKIJUA NI TARATIBU ZINASEMAJE KWA MTU ALIEWEKA PNGAMIZI ANATAKIWA AFANYE NINI ILI IWEZE KUSHUGHULIKIWA, PILI NA HASA BWANA MTINGIJOLA KWANI HAKUFUATA SHERIA INAVYOSEMA KWA UPANDE HUO, KWAMBA PINGAMIZI ILI LICHUKULIWE KWELI LINATAKIWA VIPI, AU ALITUMIA TAFASIRI ILIYOMPA NGUVU KUFANYA ALIYOFANYA. TENGA KAMA RAIS NA NDIYE ALIWATEUA, SIDHANI KAMA SHERIA INASEMA HANA NGUVU YA KUTENGUA, JE HATA KUTOA USHAURI WA KISHERIA WAKATI AKIJUA SHERIA IMEPINDISHWA. KWANINI ASIVUNJE KAMATI NA KUUNDA NYINGINE ? INAINGIA AKILINI KWELI ?
    HAWA WATU KWA PAMOJA WANAJUA WANACHOKIFANYA KWA MAKUSUDI KABISA NA SIO KWA LENGO LA KUJENGA SOKA KAMA ANAVYOPIGIA KELELE, BALI KWA MANUFAA YAO

    ReplyDelete
  4. Hilo ndio tatizo lilipo kwamba wanaopewa mamlaka ya kusimamia taratibu na kanuni,basi wao hufanya hivyo kwa maslahi binafsi. Hivi mbona watu wanamkosea mungu namna hiyo , na kujifanya wasafi sana mbele ya jamii.
    Kama wanataka tuwaumbue mbele ya jamii basi tupo tayari kwani madudu yao tunayajua sana. na itafika wakati tutayaweka wazi kweupee jamii ijue kuwa wamevikwa ngozi ya kondoo wakati wao ni chui.

    ReplyDelete
  5. Mambo yenyewe kama ndo hiyvo, hakika ni bora Tanzania ifungiwe na FIFA kuliko kuacha watu wajifanyie kama wanavyotaka. Huu ni UJINGA kabisa. nilikuwa nam"respect" kikweli Inj. Tenga lakini kwa kuachia madudu yafanyike kama ilivyotokea, amejivunjia heshima yake.

    namuomba Mhe. Waziri akazie maamuzi yake na ni bora tufungiwe kuliko ujinga unaoendelea wa wajinga wachache kwa masnufaa yao binafsi.

    ReplyDelete