Search This Blog

Friday, March 8, 2013

BAADA YA KUVURUNDA LIGI KUU: KOCHA WA JKT AJIUZULU

KOCHA wa JKT Ruvu, Charles Kilinda ametangaza rasmi kujiuzulu kukinoa kikosi cha timu hiyo kutokana na kutofanya vizuri kwenye mechi zake za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kilinda amechukua uamuzi huo, baada ya timu hiyo, kufungwa mabao 2-0 na Kagera Sugar katika mchezo wa ligi uliopigwa Uwanja wa Azam, Chamazi juzi Alhamisi.
"Nafikiri ni muda mwafaka kuchukua uamuzi mgumu, kijiuzulu ili kuinusuru timu."
"Binafsi kwa uelewa wangu timu inapopata matokeo mabaya, kocha ndiye anayepaswa kuwajibika."
"Kwa hiyo nimeona ni vema na haki kuachia ngazi aje mtu mwingine kuokoa jahazi." alisema Kilinda ambaye amekinoa kikosi cha JKT Ruvu kwa miaka sita tangu 2007/13.
Kocha huyo alisema, baada ya kutangaza rasmi kujiuzulu kinachofuata kwa sasa ni kuandika barua uongozi wa timu kuthibitisha hilo.
"Najua kwa sasa watakuwa wanasikia habari hizi kwenye vyombo vya habari. Barua nitaiwakilisha wakati wowote kuanzia sasa." alisema Kilinda.


WACHEZAJI;
"Taarifa tumezipata. Kila mtu amesikitika. Binafsi nimeumia sana. Kocha alikuwa mtu mkarimu na mwenye upendo na kila mtu pasipo kubagua."
"Kubwa ambalo amelitamka kujiuzulu kwake ni matokeo mabaya ya timu." alisema Amosi Mgisa ambaye ni mshambuliaji wa JKT Ruvu.
'Nafikiri tunapaswa kuheshimu uamuzi wake. Ndilo suala ambalo limebaki kwa sasa."
"Kila mtu ameguswa na kueleza jinsi alivyopokea taarifa hizo. Lakini kwa sasa nafikiri ni wakati kuweka nguvu pamoja na kushinda mechi zilizosalia." alisema nahodha wa timu, Hussein Bunu.
Kabla ya Kilinda kubwaga manyanga aliwahi kutamka tangu ameanza kazi ya kufunda soka hakuwahi kuwa na msimu mbaya wa ligi kama huu.
JKT Ruvu ina pointi 19 sawa na mechi ambazo imecheza na kujiweka katika nafasi ya nne kutoka mkiani.
Maafande hao wanalazika kushinda mechi saba zilizobaki na kufikisha pointi 40 ambazo haziwezi kufikiwa na timu tatu za mwisho, African Lyon, Toto African na Polisi Moro.

2 comments:

  1. haya bro, binafsi nakukumbuka saaaaana wakati unatandaza kabumbu pale yanga mkiwa wachezaji watatu wenye majina yanayofanana yaani CHARLES KILINDA,CHARLES BONIFACE,CHARLES ALBERTO mkimuuua PAN AFRICAN goli mbili kombe la mapinduzi 1982 goli la pili likifungwa na CHARLES ALBETO likigonga mwamba na kujaa wavuni JUMA PONDAMALI akiduwaaa, baada ya hapo wewe na CHARLES ALBERTO ikasemekana mmechukua meli mkawa mabaharia nakuaminia kila lakheri .

    ReplyDelete
  2. huu ni uungwana ukiona umeshindwa kujiuzulu lakini kilinda unawapa mtihani waliobaki na timu!!

    ReplyDelete