SALAAM,
JANA
na leo, zimetolewa habari tofauti kuhusiana
na kalbu ya Simba ambazo uongozi umeona ni vema uzitolee ufafanuzi kwa
lengo la kuweka rekodi sawa. Ufuatao ndiyo ufafanuzi wa taarifa hizo.
1. SIMBA KUZUIWA HOTELINI
SAA
mbili kabla ya mechi ya jana baina ya Simba na Coastal Union ya Tanga,
mmiliki wa Saphire Court Hotel alitoa taarifa kwa uongozi wa Simba
kwamba ataizuia timu isiondoke hotelini kwa vile anaidai
Sh milioni 25 na anataka alipwe zote jana.
Ikumbukwe
kwamba Simba imekuwa ikikaa hotelini hapo kwa muda mrefu sasa wakati
inapoweka kambi. Pia, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba walifanya
mkutano na wachezaji wote wa Simba katika hoteli hiyo usiku wa kuamkia
jana.
Wamiliki
wa hoteli hiyo hawakutoa taarifa yoyote kwa uongozi wakati huo juu ya
dhamira yao
hiyo.Wamiliki hao hawakutoa taarifa asubuhi ya mechi na walisubiri
mpaka wakati timu inataka kuondoka ndiyo wakachukua hatua hiyo.
Kwa
uongozi wa Simba, hatua hiyo ilikuwa ya ghafla mno. Ifahamike kwamba
kabla ya hatua hiyo, uongozi wa Simba ulikuwa umemlipa mmiliki huyo
kiasi cha zaidi ya Sh milioni 30 katika kipindi cha miezi 10 iliyopita.
Mara
baada ya mechi
dhidi ya Libolo ya Angola, Saphire walilipwa Sh milioni 15 na Simba.
Hii maana yake ni kwamba klabu yetu ina utaratibu wa kulipa madeni yake
na si watu wasiolipa kama hatua hiyo ya wamiliki wa Saphire inavyotaka
kueleza.
Uongozi
wa Simba tayari ulitoa ahadi ya kumaliza deni lote inalodaiwa baada ya
kulipwa fedha zake inazodai zinazotakiwa kulipwa wakati wowote mwezi huu
au ujao. Simba inadai zaidi ya Sh milioni 500 kwa wadai wake wawili
(Etoile du Sahel ya Tunisia na Push Mobile) na inataraji kulipwa fedha
hizo.
Itakapolipwa
fedha zake hizo, Simba itakuwa na uwezo wa kulipa madeni yake yote
inayodaiwa na watu binafsi na makampuni bado ikabaki na fedha za kufanya
mambo mengine ya kimaendeleo.
Wakati
ikisubiri ilipwe fedha zake inazodai, Simba itaendelea kulipa madeni
yake taratibu kwa kadri itakavyoweza. Ifahamike kwamba kwa sasa chanzo
kikuu cha mapato ya klabu ni fedha za mapato ya milangoni na za udhamini
wa bia ya KILIMANJARO ambazo hazikidhi mahitaji yote ya timu.
Kwa
kuzingatia nakisi hii ya mapato na matumizi, Simba SC imeanza mchakato
wa kutafuta wafadhili na wadhamini kokote walipo duniani ili kuongeza
mapato yake. Tayari mawasiliano yameanza na wenzetu wa Sunderland ya
England kupitia mradi wao wa Invest in Africa ili Simba nayo ifaidike.
Simba
SC inaomba pia umma ufahamishwe kwamba klabu ya soka kudaiwa si dhambi.
Iwapo klabu kubwa na tajiri duniani kama
vile Manchenster United, Real Madrid na Liverpool zina madeni, inakuaje
madeni ya Wekundu wa Msimbazi (tena ambayo klabu ingeweza kuyalipa yote
iwapo wadeni wake nayo wangewalipa kwa wakati) yaonekane kama kitu
kigeni?
Uongozi
unaahidi kwamba utalipa madeni yake yote kwa kadri utakavyojaaliwa.
Kwenye lugha ya kibenki, credit worthiness ya mteja inamaanisha mteja
ambaye anakopa na kulipa. Simba inapenda kusisitiza kwamba ni taasisi ya
kuaminika na yenye heshima kubwa na bado inavutia watu na taasisi
mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Hata
hivyo, uongozi wa Simba unafikiria kuchukua hatua za kisheria dhidi ya
wamiliki wa Saphire Court Hotel kwa kitendo chake cha kuwazuia wachezaji
na viongozi wa Simba hotelini kabla ya mechi ya jana.
Simba
inachukulia kitendo kile kama hujuma na kisheria kinaangukia katika
kundi la Forced Imprisonment, kwa mmiliki kuwazuia watu kinguvu.
WAMILIKI hawakutoa notisi kwa uongozi au taarifa yoyote ya mdomo au
maandishi kabla ya kuchukua hatua hiyo.
Lengo
lilikuwa ni kuchafua heshima na hadhi ya Simba kwa hoteli ambayo
imetoka kulipwa Sh. milioni 15 wiki mbili tu zilizopita. Uongozi wa
Simba SC unaapa kuilinda na kuitetea hadhi ya klabu yetu kwa nguvu zetu
zote, akili zetu zote na maarifa yetu yote.
2. WACHEZAJI, BENCHI LA UFUNDI KUFUKUZWA
KUNA
taarifa zimeenezwa pia kwamba kuna wachezaji wa Simba wamesimamishwa au
kufukuzwa kuchezea Simba. Habari hizi nazo hazina ukweli wowote
Ukweli
ni kwamba, uongozi wa Simba umetoa ruksa kwa benchi la ufundi kupanga
timu ambayo litaona inafaa kwa mechi husika. Uongozi hautaingilia, kwa
namna,njia au aina yoyote ile utendaji wa benchi la ufundi.
Hakuna
mchezaji yeyote aliyesimamishwa hadi sasa. Pia uongozi unakanusha
taarifa kuwa Daktari Mkuu wa Klabu, Cosmas Alex Kapinga, kuwa naye
ameachia ngazi. Habari hizi hazina ukweli kwani daktari huyo ana ruhusa
ya kikazi ya wiki mbili inayojulikana.
HITIMISHO
KATIKA
namna ya kipekee kabisa, uongozi wa Simba unapenda kutoa shukrani za
dhati kabisa kwa washabiki wake waliojitokeza Uwanja wa Taifa na
kuisapoti timu kwa asilimia 100. Uongozi unathamini sana mchango wa
wanachama wake na unaahidi kufanya kila unachoweza kuwarejeshea tena
furaha mioyoni mwao.
Uongozi
pia unatumia nafasi hii kuwapongeza wachezaji na benchi la ufundi ambao
walicheza mechi ya jana katika mazingira magumu. Walicheza bila ya
kufanya warm up na wakitoka kuwa wamezuiwa hotelini jambo ambalo
lingeweza kuwaondoa mchezoni.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC
imetulia sana taarifa hii, Bug up Kamwaga et al'
ReplyDeleteHapa naona mchezo wamatumizi machafu ya hela yameanza,, najiuliza je kama asingeuzwa Okwi timu ingeweka kambi wapii na ingelipa nini? Hapa kuna mpango wa matumizi machafu ya hela. Hizo kampuni bubu ulizosema ni zipi na zinadai nini?? hapa utasikia kampuni ya fulani nayo inadai ili mradi hela iishe. Hii timu inahitaji kuwa mnatoa audited accounts kila mwaka. Maana mnajiachia mno. Ndio maana makocha wachezaji mnawasajili na kuwaajili kienyeji mno kwa maslahi binafsi mwisho timu ndiyo inapata hasara. Nawaomba mfuate utaratibu wekeni hata washauri wakiuchumi wapo watakao jitolea wadau wengi wapo wanaumia kwa kutomakinika kwenu.
ReplyDeleteWe kamwaga pia mnafiki tu.......... hayo uliondika hapo ni just siasa tu lakini ukweli ni kwamba timu yetu ina hali mbaya sana na mnachojaribu ni kutudanganya ili tuone mambo yanaenda lakini hamna kitu! na mwaka huu hata nafasi ya tatu hatushiki, upuuzi mtupu.
ReplyDeleteWewe na Rage wote inabidi muchomoke hapo simba mnatuletea usiku tu, hayo madeni huwa hamlipi nyie ndio maana timu ilizuiwa hotelini.
We ni mfaiki tu, mpuuzi wewe!
nyie ni hovyo tu mipango yenu vululu vululu yaani mburulaa
ReplyDeleteJamani msimshambulie Kamwaga bure,kazi zake hivi sasa zinafanywa na Mwenyekiti kwani kila siku ndiye anayeongea na vyombo vya habari,ndiyo maana Kamwaga ameamua kuwa Msemaji wa Liverpool"Mr Liverpool"
ReplyDelete