Search This Blog

Tuesday, March 12, 2013

EXCLUSIVE: IMEFAHAMIKA TENGA NI MMOJA WA WAJUMBE YA KAMATI YA USULUHISHI WA MIGOGORO YA WANACHAMA WA FIFA INAYOKUJA TANZANIA KUTATUA MGOGORO WA SERIKALI NA TFF. JE HAKI ITATENDEKA?

Wakati Tanzania ikiwa kwenye hatari ya kufungiwa na shirikisho la soka duniani kwa mujibu wa TFF kutokana na mgogoro unaoendelea baina ya serikali na shirikisho la soka nchini. Imefahamika kwamba Raisi wa shirikisho la soka nchini Leogdar Tenga ni mmoja wa kamati ya vyama vya soka duniani inayoshughulikia misuguano/migogoro inayohusisha wanachama wa FIFA.
Hivi karibuni kupitia TFF, ilitolewa taarifa kwamba FIFA ingetuma wajumbe wake kutoka kwenye kamati ya kushughulikia migogoro ya wanachama kuja kusuluhisha au kutatua mgogoro unaoendelea hivi sasa kwenye soka la nchi hii.
 SWALI TATA
Leogdar Tenga kama mmoja wa mjumbe wa kamati ya FIFA ya kushughulikia migogoro ya wanachama wake, ataweza kuvaa kofia mbili ya uraisi wa TFF na uanachama wa kamati ya usuluhishi na kuweza kutenda haki kwa pande mbili zinazokinzana kwenye mgogoro huu?
Chairman
Senes ERZIK Turkey Turkey
Deputy Chairman
Mohamed RAOURAOUA Algeria Algeria
MemberS
Rafael CALLEJAS Honduras Honduras
Costakis KOUTSOKOUMNIS Cyprus Cyprus
Peter GILLIERON Switzerland Switzerland
Leodegar TENGA Tanzania Tanzania
Michael VAN PRAAG Netherlands Netherlands
Carlos Alberto CHÁVEZ Bolivia Bolivia
Justino COMPEAN Mexico Mexico
Hamidou DJIBRILLA Niger Niger
Ugen Tsechup DORJI Bhutan Bhutan
Hachem HAYDAR Lebanon Lebanon
Sergio JADUE Chile Chile
Francisco LAY Timor-Leste Timor-Leste
Adam MTHETHWA Swaziland Swaziland
Walter NYAMILANDU Malawi Malawi
Toetu PETANA Samoa Samoa
Anton SEALEY Bahamas Bahamas
Kuniya DAINI Japan Japan
Giancarlo ABETE Italy Italy
Kwesi NYANTAKYI Ghana Ghana
Nikolai TOLSTYKH Russia Russia

13 comments:

  1. Haki itatendeka tu. kwa taratibu za kisheria kama kuna mgongano wa kimaslahi muhusika anakaa pembeni katika shauri husika. tusubiri FIFA wafanye kazi yao na tusiingize majungu katika hili.

    ReplyDelete
  2. Mimi namwamini sana Tenga,Tenga kabadilisha sana soka letu na ni mtu pekee aliyelifanya soka la Tanzania lisichezewe mahakamani kila wakati kama ilivyo miaka iliyopita.

    Tenga kasababisha soka la Tanzania liwe na heshima yake ya kipekee lakini pia Tenga si mtu wa majungu na ndio maana FIFA wamemwamini na kumpa nafasi hiyo ya kusululisha migogoro ya kisoka Duniani.

    Tenga tangu mwanzo alikuwa akisimamia maneno yake na alimweleza ukweli waziri kuwa kapotoshwa na serikali haikuweza kukubaliana nae, labda kuna maslahi ya watu yameguswa ktk uchaguzi ule,

    nachokiamini toka kwa Tenga ni kwamba atasimamia ukweli na kikawaida ukweli ndio humweka huru mtu daima.

    Tenga kwa uwezo alionao atatenda haki kwani ni mtu wa soka na anapenda soka na amelionyesha hili hata ktk kipindi chake alipokuwa madarakani.

    Naelewa kuwa mtu kama Dauda asiweze kukubaliana na hili lakini ukweli ndio huo.

    ReplyDelete
  3. Shaffii kwa jinsi nivyoelewa hiyo ni kamati ambayo, imeundwa kusuluhisha migogoro itakapotokea. kwa hili la kwetu Tenga nina uhakika kwa jinsi ninavyomjua atakaa pembeni watu wafanye kazi, mtu huwezi jichunguza. lakini nimesikia kama ile kamati haiji tena, hadi serikali issingilie

    ReplyDelete
  4. Mmmmmmh shughuli ipo maendeleo ya kweli cjui..............!

    ReplyDelete
  5. mimi tatizo kubwa hapa ni namna naibu waziri wahabari utamaduni na michezo lugha anayoitumia ktk sakata hili si ya kiongozi,inaonekana kama wanaonyeshana ubabe na TFF wakati ilikuwa issue ndogo sana,hata yeye ameonesha waziwazi yupo upande wa jamal malinzi,kwani lazima jamal malinzi agombee tu kuongoza mpira? hata alipokuwa yanga hakuna jipya alilofanya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. mkubwa, nakubaliana na mawazo yako hivi huyu, makalla alishawahi kupata shule ya uongozi kweli. hata kama ni shabiki wa mtu kwa kofia yake anatakiwa kufikiri kwanza ndio atoe ripoti zake, anaropoka tu mara mdau mara serikali, ameikuza issue ndogo, tusikubali kuburuzwa kwa utashi wa mtu eti tufungiwe FIFA, sasa mpira gani bila FIFA na kwa issue ipi, hii ya Malinzi ambaye ameshindwa kuthibitisha uzoefu wa miaka mitano? masihara haya jamani

      Delete
  6. naungana moja kwa moja na mdau alietangulia hapo acheni fifa wafanye kazi yao penye dosari pataonekana tu majungu na umbea hauta tufikisha popote

    ReplyDelete
  7. Hapo ndipo ule msemo wa nabii hakubaliki nyumbani kwao,wakati sisi huku tunamponda Tenga kutokan na fitna zetu za kijinga,wenzetu walioendelea wanamuamini sana na wanamkubali kutokana na hekima,busara ,elimu,uzoefu na upeo alionao kwenye mambo ya uongozi hususan soka.Huyu ni mtu mwenye upeo na hatakubali kuwa na conflict of interest ingawa ukweli atauweka hadharani sababu yeye atakuwa sehemu ya pande zinazosuluhishwa katika mgogoro huu.Hivi mtu kama Amos Makala anaweza kusimama mbele ya watu wenye akili timamu na kumponda Tenga halafu watu hao wakamwelewa?hivi hadhi ya Makala pamoja na uwaziri wake inamfikia Tenga hata nusu kweli?mtu ambaye anatukanana na watu walioko chini yake kimadaraka badala ya kuwaita ofisini?mtu ambaye anazungumzia jambo la sekta anyoiongoza halafu anadai anaongea kama mdau?halafu Angetile anapomkosoa kwa kuongea kama mdau vyombo vya habari vinaponda Angetile kwamba anabishana na serikali wakati serikali yenyewe imejivua uwaziri na kuongea kama mdau?.Muda si mrefu watanzania tutajutia kosa tunaliotaka kufanya la kuiondoa TFF toka kwa walioucheza mpira(Tenga) na kuipeleka kwa wanasiasa,wacheza gofu,mapromota wa ngumi na wadau wa kriketi.Tukumbuke wenzetu waliofanya kazi kubwa mwaka 2004 ya kuirudisha TFF mikononi mwa waliocheza mpira.

    ReplyDelete
  8. kwani wewe shaffii huina imani na tenga kuwa msuluhishi wa hili?? binafsi sio ubaya wa tenga ktk hili na nakumbuka kasema kabisa kama wewe mtu wa mpira iweje muwaogope fifa, ki ukweli waziri kashauriwa vibaya ktk hili na hata tukifungiwa athari zake ni kubwa kwa vijana wanovuja majasho leo hii viwanjani, hili swala linahitaji busara tu na kusikilizana na kuheshimiana, namwamini sana mweshimiwa waziri namwamini sana rais tenga sidhani kama tutakuja kufikia huko mnakosema kufungiwa.

    ReplyDelete
  9. Shafii dauda mbona hujaweka story ya kutaka kupigwa siku ilipocheza simba na costal union? Acha kuidharau simba

    ReplyDelete
  10. shafii unabana, ukweli ni kwamba siasa ni mchezo mchafu, tusiuingize ktk vyama vingine, , kama ulifanikiwa kupitia blaa blaaaa, hapa ni kisomi tu!!!! TFF NENDA NA KATIBA YA FIFA TUNAHITAJI VIONGOZI WENYE MAAMUZI MAGUMU ILI TUENDELEE.

    ReplyDelete
  11. tatizo tanzania tukubali tukatae watu tupo kibinafsi na kimaslahi,ukweli uliopo ni kwamba uongozi ukibadilishwa wa TFF ujue na akina Wambura,Kayuni na Osiah ndio mwisho wao pale na ndio mana Angetile ata acha kulumbana kwani anatetea ugali wake na ndio mana anang'ang'ania pasiwepo mabadiliko ya uongozi

    ReplyDelete
  12. mimi niseme tu TENGA TFF si yake na kafika hapo kwasababu ya watanzania waliokua wanamtakia mema na heri toka mwanzo alipoingia kama rais na akumbuke kua usaliti anao ufanya utamwandama na kama tanzania ikija fungiwa lawama zote ni zake na ajue mpira ndo unafanya wengine tusahau umasikini,kukatika kwa umeme na foleni barabarani

    ReplyDelete