Search This Blog

Tuesday, March 12, 2013

HUKU AKITEGEMEWA KUPATA MTOTO NA DADA YAKE BALOTELLI - OBAFEMI MARTINS ANUNUA MKATABA WAKE NA LEVANTE ILI AHAMIE MAREKANI

Mchezaji wa zamani wa Inter na Newcastle Obafemi Martins ameripotiwa kulipa kiasi cha €3 million kununua mkataba wake na Levante ili aweze kujiunga na Seattle Sounders. Martins ambaye alijiunga na Levante mwezi September akiwa huru na akasaini mkataba wa miaka miwli kabla ya kuwa mfungaji bora wa klabu hiyo msimu huu akifunga mabao 7 katika mechi 21 za La Liga. Na sasa mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 ameamua kuelekea MLS.
Kutoka Reuters:
"Jioni hii, Martins amelipa fedha za kununulia mkataba wake kama ambavyo kipengele cha kuvunja mkataba wake na Levante unavyoelekeza.," taarifa iliyotolewa na klabu hiyo ya Spain.
Media za kispanish zimeripoti fedha hizo ni kiasi kisichopungua 3 million euros ($3.9 million).
Akaunti ya Twitter  inayodaiwa kumilikiwa na Martins, ambaye aliigharimu Rubin Kazan €17 million in 2010, na alikaririwa na mtandao rasmi wa ligi kuu ya Marekani kwamba anaenda kujiunga na Seattle.


Ingawa kwa hakika Seattle watamlipa Martins kwa kununua mkataba wake. Martins ameelezea matamanio yake ya kuihamishia familia yake US. Pia ameripotiwa kwamba anategemea kupata mtoto na dada wa mtukutu Mario Balotelli aitwaye Abigail.

No comments:

Post a Comment