Search This Blog

Tuesday, March 12, 2013

AC MILAN KUFUATA NYAYO ZA CHELSEA KUICHINJA BARCA MBELE YA MASHABIKI WAO 90,000?

FC Barcelona vs AC Milan imekuwa moja ya mechi nzuri sana katika miaka ya hivi karibuni kutokana na ushindani mkubwa unaokuwepo. Kutoka msimu wa 2000/01 Barcelona na Milan zimekutana mara tano kwenye dimba la Nou Camp pekee, Barca wakishinda mara 2, Milan mara moja na wakitoka sare mara mbili. AC Milan katika historia yao wameshacheza mara 14 kwenye dimba la Nou Camp, wakishinda mara nne, wakifungwa mara 6, na mechi nne zikiishia kwenye suluhu. 

Leo usiku Milan wanaingia Nou Camp wakiwa mbele kwa ushindi wa 2-0, lakini watakuwa bila mchezaji wao mahiri Pazzini ambaye aliumia hivi karibuni kwenye Serie A, Barca kwa upande wao wamepata faraja baada ya nahodha msaidizi Xavi Hernandez kupasi vipimo vya afya na leo asubuhi alifanya mazoezi na timu.

Je yakiwa yamebakia takribani masaa mawili kabla ya kipenga kupulizwa Milan wataweza kuhimiri mikimiki ya Lionel Messi na wenzie waliojeruhiwa wakiwa kwenye mbele ya mashabiki wao wapatao 90,000 au Barca watapa aibu nyingine ya kutolewa kwenye UCL nyumbani kwao kama ilivyokuwa msimu uliopita dhidi ya Chelsea

No comments:

Post a Comment