Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Coastal Union iliyochezwa juzi
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 36,820,000 kutoka na
watazamaji 6,284.
Viingilio
katika mechi hiyo namba 138 iliyomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi
wa mabao 2-1 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000
huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 8,265,752.45 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 5,616,610.17.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 4,202,924.97,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 2,521,754.98, Kamati ya Ligi
sh. 2,521,754.98, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
1,260,877.49 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 980,682.49.
Jana zilitoka taarifa kwamba Watazamaji
7,412 walishuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga
na Toto Africans lililochezwa jana (Machi 9 mwaka huu) Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam na kuingiza sh. 42,508,000.
No comments:
Post a Comment