Search This Blog

Saturday, March 2, 2013

HATIMAYE DORTMUND WATHIBITISHA LEWANDOSKI ATAONDOKA KWENYE TIMU YAO

Robert Lewandowski ataondoka Borussia Dortmund katika kipindi cha miezi 18 ijayo baada ya kukataa mkataba mpya, kwa mujibu wa mkurugenzi wa michezo wa Dortmund Michael Zorc.

Lewandowski, ambaye amekuwa akihusishwa sans na kujiunga na na Bayern Munich na Manchester United, yupo kwenye mkataba na mabingwa wa Bundesliga mpaka mwaka 2014 lakini Zorc  ameiambia SKY TV ya Ujerumani kwamba mchezaji huyo hatosaini mkataba mpya.

Wakala wa mchezaji huyo amemtaarifu Zorc kwamba mteja wake hana mpango wa kuendelea kubaki Dortmund, akimaanisha kwamba mpoland huyo ataondoka kwenye klabu hiyo.

"Anaweza kuondoka mwishoni maw msimu au akabaki kwa mwaka mwingine," alisema Zorc.

Huko nyuma, gazeti la mini Munchner Merkur liliripoti kwamba dili limeshakamilika kati ya Lewandoski na Bayern, na angetangazwa kujiunga na Bayern kwenye mechi ya jana usiku kati ya Dortmund na Bayern. Japokuwa hakukuwa na tangazo lolote kuhusu usajili na huku Bayern wakikanusha kupitia mkurugenzi wao wa michezo Mathias Sammer kwamba hawatozungumzia tena suala la tetesi zisizo za ukweli za usajili wa Lewandoski.


No comments:

Post a Comment