Search This Blog

Saturday, March 2, 2013

AZAM FC WATUA NA VYAKULA VYAO JUBA SUDAN

AZAM FC imenunua chakula chake binafsi kwa hofu ya hujuma wakati ikitarajiwa kuwasili leo Jumamosi kujiandaa na mechi dhidi ya Al Nasri kesho Jumapili.

Uongozi umenunua mchele mjini Nairobi, Kenya wakati mchele mwingine unatarajiwa kuletwa leo Jumamosi mjini Juba na viongozi wengine wa Azam.

Hata hivyo jumla ya kilo 30 za mchele zilinunuliwa Juba kwa ajili ya chakula cha wachezaji. Kwa mujibu wa Watanzania wanaoishi mjini Juba walisema, tatizo la kuwekeana sumu katika chakula mjini Juba ni suala la kawaida hivyo inabidi kuwa makini muda wote.

 Watu wa hapa Juba bado wana tatizo la kumalizana kwa kuwekeana sumu katika chakula, hata sisi wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa hatupikiwi chakula cha pamoja, sisi hununua chakula chetu na kila mtu hujipikia, alisema Kassim Matokeo ambaye ni Mtanzania anayefanya kazi katika ofisi za Umoja wa Mataifa hapa Sudan ya Kusini.

Tayari viongozi wa Azam waliotangulia kwa ajili ya kuandaa mazingira hapa Juba wameshaandaa utaratibu kwa ajili ya kupika wenyewe chakula hicho cha wachezaji ili kuepuka kuhujumiwa.

Azam itakabiliana na Al Nasri katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika. Katika mechi ya kwanza Azam ilishinda 3-1 Dar es Salaam.

Msafara wa Azam utakaokuwa na viongozi na wachezaji 20 utawasili saa 8:20 mchana ikitokea Dar es Salaam kupitia Nairobi.

Hali ya hewa hapa Jua ni jua na joto kali linalofikia nyuzi 40 ingawa wenyeji wanadai huongezeka zaidi ya hapo. Mji wa Juba unatumia umeme wa majenereta.

Uongozi wa Azam umeikataa Hoteli ya South Sudan ambayo ilikuwa imeandaliwa na wenyeji wao.

Mratibu wa Azam, Florian Kaijage akiwa na kocha msaidizi wa Azam, Kally Ongala waliikataa hoteli hiyo na kuchukua Hoteli ya Rainbow.

Gharama za hoteli hapa Juba zipo juu kwani hoteli zipo chache. Chumba kinaanzia dola 100(sh.160,000) kwenda juu.


SOURCE: GAZETI LA MWANASPOTI

No comments:

Post a Comment