Search This Blog

Saturday, February 23, 2013

YANGA WALIVYOKATA NGEBE ZA AZAM FC LEO JIONI

 Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete, akijilaumu baada ya kukosa bao la wazi.
 Mshambuliaji wa Yanga Jerry Tegete (kuli) akijaribu kumchambua kipa wa Azam Fc, Mwadin Ally, wakati wa mchezo huo, ambapo Tegete alikosa baada ya kipa huyo kuudaka mpira huo.
 WATANI WA JADI BWANA!!!!, Mashabiki wa Yanga, wakiwakebehi watani wao Mashabiki wa Simba waliokuwa wakiishangilia Azam Fc, kwa Bango lenye Ujumbe huu. ''Msomaji soma mwenyewe''.
 Kikosi cha kwanza cha Yanga kilichoanza.
 Sehemu ya mashabiki wa Yanga, waliojitokeza kuishangilia timu yao leo, ambao wanakadiliwa kuwa kama 25,0000 hivi.
Kikosi cha Azam Fc kilichoanza. 
 
 Beki wa Yanga, Nadir Haroub 'Canavaro', akimkabili mshambuliaji wa Azam, Kipre Tchetche, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara
 
Wachezaji wa Yanga wakimpongeza Niyonzima baada ya kutupia bao.(PICHA KWA HISANI YA SUFIANI MAFOTO)

10 comments:

  1. Shaffih, katika picha hapo juu naomba kuuliza kwa nini mashabiki wakadiriwe kufikia 25,000? Kwani vishina vya tiketi za mashabiki waliokata tiketi hazitoi idadi kamili ya walioingia uwanjani? Naomba mnisaidie jamani.

    ReplyDelete
  2. hata wakikupa idadi kamili we utafaidika na nini? shaffi amekwambia hilo ni kadilio ukitaka kujua idadi kamili watafute wasimamaizi wa mchezo

    ReplyDelete
  3. Habari imesema washabiki wa yanga wanakadiliwa kufikia sio idadi kamili ni makisio tu kutokana na sehemu waliyokaa na wingi wao.Hayo ni makisio tu katika kunogesha habari

    ReplyDelete
  4. utasikia makusanyo mil 200 tu. vilabu vinaumia kweli

    ReplyDelete
  5. Ndugu anonymous,kwa uelewa wangu mdogo,mpiga picha hiyo hapo juu,amekadiria mashabiki wa Yanga waliokuwa au kufika uwanjani na si kwamba idadi halisi ya mashabiki wote walioingia uwanjani.


    ReplyDelete
  6. I ngawa mi sio Shaffih naweza kujibu kuwa suala la tiketi ngapi zimeuzwa ni suala linaloweza kupatikana toka TFF baada ya kufanya mahesabu halisi kwamba ni itabu vingapi ya tiketi ilisambazwa ktk vituo vya mauzo na vingapi imeuzwa na idadi iliyobaki.Makisio ya Shaffih ni idadi ya viti iliyopo ktk majukwaa.

    ReplyDelete
  7. Jana mashabiki watakuwa walifika 50000,coz watu wengi wakikaa kwenye ngazi na corrido kuogopa jua.... uwanja ulijaaa.

    ReplyDelete
  8. YAnga wanatisha sana wamejiandaa viziri!hongereni sana!keep it up!

    ReplyDelete
  9. love u yanga nipe raha nizisahau man u na arsenal

    ReplyDelete
  10. kaka huyu ni muandishi wa habari anatoa taarifa ya mchezo vishina na yeye wapi na wapi...?
    nadhani umesikia taarifa kamili toka tff waliingia wangapi na wamepata nini...?

    ReplyDelete