Search This Blog

Sunday, February 24, 2013

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA SC 0 -1 MTIBWA SUGAR FULL TIME

Dk 90+5 FULL TIME! SIMBA 0-1 MTIBWA.

Dk 85 RED CARD....! Juma Nyosso wa Simba anaonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Vincent Barnabas wa Mtibwa. Simba 0-1 Mtibwa.

Dk 84 Mtibwa imefanya mabadiliko, ametoka Hussein Javu ameingia Juma Liuzio

Dk 82 Sunzu anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kuingilia mpira wa Mtibwa uliokuwa unaanza.

Dk 69 Said Mkopi wa Mtibwa anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Mrisho Ngassa wa Simba.

Dk 65 Simba imecharuka inalishambulia zaidi lango la Mtibwa. Simba 0-1 Mtibwa.

Dk 58 Simba imefanya mabadiliko, ametoka Chanongo ameingia Mrisho Ngassa.

Dk 58 Simba imefanya mabadiliko, ametoka Chanongo ameingia Mrisho Ngassa.

Dk 51 Nditi anaonyeshwa kadi ya njano baada kumlalamikia mwamuzi kupita kiasi baada ya kugongana na Chollo.

Dk 51 Beki wa kulia wa Simba, Nassor Masoud 'Chollo' anaumia mkono baada ya kugongana na Shaaban Nditi wa Mtibwa. Mpira unasimama kwa muda. Simba 0-1 Mtibwa.

Dk 50 Simba imefanya mabadiliko, ametoka Haruna Moshi 'Boban' ameingia Amri Kiemba.

Dk 49 Mtibwa inafanya mabadiliko, ametoka Mnyate, ameingia Ally Mohamed.

Dk 48 Chanongo wa Simba anaichambua ngome ya Mtibwa na kupiga shuti kali nje ya lango la Mtibwa.

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA!

Dk 45 HALF TIME! SIMBA 0-1 MTIBWA.

Dk 45 Jamal Mnyate wa Mtibwa anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kulumbana na mwamuzi kuhusu faulo aliyochezewa Kiggi.

Dk 45 Kiggi Makassy wa Simba anaangushwa nje kidogo ya eneo la hatari la Mtibwa. Faulo inapigwa na mpira unatoka nje.

Dk 41 Simba imefanya mabadiliko, ametoka Ramadhan Chombo ameingia Kiggi Makassy. Chombo anatoka moja kwa moja kwenda vyumba vya kubadilishia nguo bila ya kwenda benchi.

Dk 40 Kipa wa Mtibwa, Hussein Sharrif 'Cassilas' anaumia baada ya kugongwa na Haruna Chanongo wa Simba.

Dk 28 Sunzu anashindwa kuunganisha kwa kichwa krosi ya Haruna Chanongo. Mpira anaopiga unatoka nje. Simba 0-1 Mtibwa

Dk 23 Mshambuliaji wa Mtibwa, Hussein Javu anapiga shuti kali langoni kwa Simba baada ya kuwazidi mbio mabeki Juma Nyosso na Komanbil Keita.

Dk 18 Kipa wa Simba, Juma Kaseja anaumia baada ya kugongana na Jamal Mnyate wa Mtibwa.

Dk 17 GOOO....! Salvatory Ntebe anaipatia Mtibwa bao la kwanza akimalizia pasi ya Vincent Barnabas. Simba 0-1 Mtibwa.

Dk 13 Kiungo wa Mtibwa, Rashid Gumbo anakumbana na mchezaji wa Simba na kuumia. Anatibiwa na mpira unaendelea.

Dk 10 Mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu anaonekana hayupo katika kiwango chake kwani anaonekana hana kasi pia anapoteza pasi nyingi anazopewa.

Dk 7 Mpira umepooza sana, timu bado zinasomana.

Dk 2 Beki Shomari Kapombe wa Simba anapiga shuti kali linalotoka juu ya lango la Mtibwa baada ya kupokea pasi ya Amir Maftah. Simba 0-0 Mtibwa.

Dk 00 MPIRA UMEANZA!

Simba Line Up: Juma Kaseja, Nassoro Masoud 'Chollo', Amir Maftah, Juma Nyosso, Komanbil Keita, Shomari Kapombe, Ramadhan Chombo, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi 'Boban', Haruna Chanongo

Mtibwa Line Up: Hussein Sharrif 'Cassilas', Said Mkopi, Issa Rashid, Salvatory Ntebe, Salum Sued, Shaaban Nditi (C), Jamal Mnyate, Rashid Gumbo, Hussein Javu, Shaaban Kisiga, Vincent Barnabas.

10 comments:

  1. Kila la heri. Haki itendeke mshindi apatikane kihalali

    ReplyDelete
  2. Jinsi unavyoihofia Yanga,ebu check iyo Update ya DK28 inakuwaje wanacheza mtibwa na simba lakini unatoa matokeo ya yanga na simba unajitabiria kichapo...

    ReplyDelete
  3. Dk 28 Sunzu anashindwa kuunganisha kwa kichwa krosi ya Haruna Chanongo. Mpira anaopiga unatoka nje. Simba 0-1 Yanga. Hahahahaaaaa kweli we ni shabiki wa yanga

    ReplyDelete
  4. Ngassa yukuwapi leo? Anasugua benchi nini..

    ReplyDelete
  5. Angalia dk ya 28 eti simba 0 yanga 1.. Au kwasababu umekaa jukwaa la yanga?

    ReplyDelete
  6. Kaka umeandika simba 0- yanga 1, naomba urekebishe, ni mtibwa, mkubwa.

    ReplyDelete
  7. kaka rekebisha dak.28 hapo sio yanga hao ni mtibwaaaa

    ReplyDelete
  8. hongera san mtibwa kweli mnajua kutandaza kabumbu,wekundu wamepoteana bora wasiende Angola mechi ya marejeano.

    ReplyDelete