Search This Blog

Thursday, February 14, 2013

"SIMON MSUVA NI HATARI - NDIO NGASSA MPYA WA YANGA"

BEKI wa Prisons ya Mbeya, Henri Mwalugala amekiri kuwa winga Simon Msuva ni msumbufu na kukiri alimweka kwenye wakati mgumu wakati timu yake ilipocheza na Yanga.

Mwalugala anayemudu nafasi ya beki wa kushoto alisema "Nafikiri Msuva kwa sasa amekaa vizuri."
"Nafikiri ukiwatizama Yanga kwa sasa wanamtumia sana winga huyo kujenga mashambulizi yao kupitia pembeni.
"Naamini Yanga imemrejesha Mrisho Ngassa mwingine."
Beki huyo alisema kwa mtazamo wake haoni kama Yanga ina sababu yakumsajili Mrisho Ngassa wa Simba wakati Msuva yupo.
Mwalugala akielezea jinsi timu hizo zilipokutana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam amekiri kuwa alishindwa kumzui.
"Kocha alivyoona dogo ananisumbua alinibadilisha kucheza kulia badala ya kushoto."
Alisema badiliko hilo lilikuwa na lengo la  Aziz Sibo aliyekuwa anacheza kulia kwenda kushoto kumkaba Msuva asiGlete madhara. Yanga ilishinda mabao 3-1.

No comments:

Post a Comment