Search This Blog

Thursday, February 14, 2013

"SIDHANI KAMA TUTABAKI LIGI KUU" - KOCHA WA AFRICAN LYON


ALIYEKUWA kocha wa Zanzibar Heroes Salum Bausi ameweka wazi kuwa itakuwa miujiza kwake kuibakisha African Lyon  Ligi Kuu msimu ujao.
Kocha huyo aliyeiwezesha Heroes kushinda nafasi ya tatu kwenye michuano ya Chalenji iliyofanyika jijini Kampala Uganda mwaka jana na kujinyakulia kitika cha dola 10,000.
Alisema kwa jinsi alivyoiona Lyon ikicheza mechi mbili za ligi dhidi ya Prisons na Yanga ni kazi pevu kwake kuibakisha.
"Timu haieleweki. Haina misingi ya kiuchezaji. Kila mtu anacheza anavyojisikia." alisema Bausi
Bausi alisema alitua kukinoa kikosi hicho siku tisa zilizopita na kuambiwa timu hiyo ilikuwa ikifundishwa na kocha Pablo Veles wa Argentina.
"Nafikiri ndiye anayestahili kubeba lawama hizi. Timu haina stamina wala pumzi. Wachezaji wanaanguka hovyo."
Kocha huyo alisema kwa sasa ni vigumu kuanza kuijenga timu wakati ligi ndiyo inaishia ukingoni.
"Hakuna timu inayokubali kufungwa kwa sasa. Nafikiri kama itakuwa haitafuti nafasi yakukimbia kushuka daraja basi kutwaa ubingwa."
Alisisitiza kuwa kazi ambayo ipo mbele yake ni mzito na kuomba ushirikiano kutoka kwa viongozi, wachezaji na mashabiki.

No comments:

Post a Comment