Search This Blog

Thursday, February 14, 2013

KOCHA WA COASTAL UNION: TUKIFUNGWA NA OLJORO A RUVU NAACHA KAZI


KOCHA wa Coastal Union, Hemed Morocco ameweka wazi kuwa endapo anafungwa mechi mbili zijazo dhidi ya Oljoro JKT na Ruvu Shootiga atabwaga manyanga.
Morocco alisema hayo baada ya timu hiyo kupata pointi moja Kanda ya Ziwa, kwa kutoka suluhu na vibonge Toto African na kufungwa bao 1-0 na Kagera Sugar.
Alisema yeye pamoja na kocha msaidizi Ally Kidi wamejitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha timu inafanya vizuri lakini baadhi ya wachezaji hawana nia njema na klabu hiyo.
"Inavyoonekana kuna wachezaji hawana nia nzuri na timu yao. Kwa sababu hawataki kubadilika."
"Kwa hiyo siwezi kufanya kazi kwenye mazingira hayo hata siku moja. Kama tatizo ni mimi waniambie."
Kocha huyo alisema; "Kama timu itashindwa kufanya vizuri mechi mbili zijazo nafikiri sitatangaza kujiuzulu."
Coastal Union imecheza mechi nne za mzunguko wa pili wa ligi na kutoka sare mbili dhidi ya Prisons na Toto African. Imeshinda dhidi ya Mgambo JKT na kupoteza na Kagera Sugar. 

1 comment:

  1. saf sana na hii ndo maana halis ya uwajibikaj jitume ufaid

    ReplyDelete