Search This Blog

Wednesday, February 13, 2013

SIMBA WAANZISHA MAHUSIANO NA SUNDERLAND YA ENGLAND

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Simba, Rahma Al Kharusi akiwa na Mwenyekiti wa Sunderland ya England, Ellis Short baada ya kukutana jana kwenye hoteli ya Hayat jijini Dar es Salaam.

Baada ya kukutana, wawili hao walijadili kuhusiana na klabu hizo mbili kuanzisha uhusiano wa kibiashara pamoja na mafunzo na Simba imepata mwaliko.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Short alisema ushawishi wa Malkia wa Nyuki umechangia yeye kutoa mwaliko huo na anaamini timu zote zitafaidika.
"Mazungumzo yetu na Rahma yalikuwa mazuri sana, nimefarijika na ninaamini mwaliko niliotoa utakuwa mwanzo wa uhusiano mzuri kwa kuwa mwanamama huyu amenishawishi," alisema.
Malikia wa Nyuki ataiongoza Simba nchini England mwezi Machi ambako watatembelea viwanja vya Sunderland ikiwa ni pamoja na kujifunza uendeshaji wa klabu.
Awali Simba, ilijulikana kwa jina la Sunderland.

6 comments:

  1. Naamini huu ni mwanzo mzuri mengi yanakuja nawatakieni kila la kheri simba

    ReplyDelete
  2. Mbele twasonga tuweke tofauti zetu pembeni.....Simba imara

    ReplyDelete
  3. wazee wa ndala sijui wanajisikiaje, kwa pamoja simba kanyaca twende ila tuweke siasa pembeni tuijenge simba ya kisasa

    ReplyDelete
  4. TUKAJIFUNZE KWA AZAM FC HAPA HAPA DSM KABLA YA KWENDA ENGLAND AMBAKO NI MBALI SANA

    ReplyDelete
  5. tumkabidhi malkia wa nyuki timu,rage aendelee na siasa kwa kuwatumikia wana tabora!

    ReplyDelete