Search This Blog

Wednesday, February 13, 2013

HATMA YA SOKA LA BONGO,BAADA YA MVURUGANO WA MAAMUZI YA KAMATI YA UCHAGUZI YA KUWAENGUA BAADHI YA WAGOMBEA.

-->

Huu ni mwaka 2013,ukirudi nyuma kwa miezi minne yaani mwezi wa 11 mwaka 2012,yalifanyika mashindano ya Soka kwa Timu za Taifa kutoka Ukanda wa Africa Mashariki na Kati,maarufu kama Challenge.
Mmoja wa washiriki wa michuano hiyo iliyomalizika kwa wenyeji Uganda kuitwaa,ni Timu ya Taifa ya Tanzania Bara,ambao walitolewa katika hatua ya nusu fainali na ndugu zao Tanzania Visiwani.
Kitendo cha Timu Zote mbili yaani Tanzania Bara na Visiwani kufika nusu fainali,kilikuwa furaha tosha kwa Watanzania wote kwa ujumla katika kipindi cha mashindano hayo.
Pia,Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars,hivi karibuni imecheza mechi tatu za kirafiki,ambapo mchezo wa kwanza imeshinda bao 1-0 dhidi Zambia,mechi ya pili ilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Ethiopia wakati wiki mbili zilizopita imeshinda goli moja kwa bila dhidi ya Mabingwa wazamani wa Africa Cameroon.
Matokeo ya mechi hizi ukijumuisha na hatua zilipofikia timu za Taifa za Tanzania Bara na Visiwani,yamekuwa tumaini jipya la kufufuka kwa soka la Tanzania na hatimaye kufanya vyema katika michezo tofauti ikiwemo ya kufuzu Mataifa ya Africa.
Wakati Watanzania wakiunganisha Sara zao kuliombea Soka la nyumbani,Kamati ya uchaguzi na kamati ya Rufani ya uchaguzi mkuu wa TFF na Bodi ya Ligi wameibuka na jambo jipya lakukatisha tamaa juu ya mafanikio ya Soka la Bongo.
Kamati hizo  zimetumia sababu dhaifu,kuwaengua baadhi ya wagombea wa nafasi tofauti katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Mwezi Feb 22 na 24,akiwemo mgombea wa nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo la Soka Nchini Jamal Malinzi,kwa kukataa kusaini katiba ya mabadiliko ya leseni ya Ligi na kutokuwa na uzoefu wa uongozi  kwa miaka 5
Maamuzi haya yanaonesha wazi nia ya kuwabeba baadhi ya wagombea kwa kuwatengenezea mazingira ya kushinda uchaguzi bila kupingwa,hii ni aibu kwa wadau husika hasa katika wakati huu ambapo kila mtu anafahamu kinachoendelea kutokana na kuwepo kwa uwazi na ukweli.
Aidha Maamuzi haya yanalenga kurudisha nyuma maendeleo ya Soka la Bongo,kwa kuwa baadhi ya wagombea walioenguliwa,pengine walikuwa na mipango thabiti ya kuliinua Soka hili na kulifikisha mbali zaidi ya hapa.
Katika kuonesha kuwa kitendo hiki si haki na sio cha kiungwana,Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Amos Makala,ametoa tamko kali la kuitaka kamati ya Uchaguzi ya TFF kusimamisha  shughuli za uchaguzi huo adi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi,ikiwa pamoja na kuwarudisha wagombea walioenguliwa kimakosa.
Kama ninafikiria vyema,basi ninaamini kuwa maamuzi ya kamati hii yaliyomshangaza kila mpenda Soka na kuwavunja moyo waliokuwa njiani kupenda Soka,ni msukumo kutoka kwa baadhi ya wagombea wanaotaka madaraka kwa hali na mali.
Hii ni hali ya hatari kwa hatma ya Soka la bongo ambalo lilianza kuchanua,kwa kuwa uzoefu unaonesha kuwa mtu anayetumia nguvu ya ziada kupata uongozi,huwa hayupo kwa maslahi ya Taifa isipokuwa maslahi yake binfasi kama ilivyo kwa baadhi ya Viongozi wa Siasa Nchini na nchi za jirani.
Mimi binafsi ninaamini wakati muafaka na sahihi kwa Watanzania kukemea mambo haya yaliyopitwa na wakati ni sasa,na sio baada ya maamuzi na mbinu za ya kurudisha nyuma Soka kufanikiwa.
Sote tunafahamu kuwa Mpira wa Miguu ni Mchezo unaoongoza kwa kupendwa Duniani kote,na pia ni mchezo unaotoa ajira nyingi kwa Vijana wenye kipaji cha Mchezo huo kiasi cha wachezaji wengine kuingia kwenye orodha ya watu matajiri.
Kutokana na hilo,Wadau wote wa Soka na Michezo kwa ujumla nchini,tuungane kuhakikisha jitahada za kukuza Soka la Bongo lenye vijana wenye ndoto za kufanikiwa kitaifa na kimataifa na hatimaye kuitangaza Nchi zinafanikiwa kwa kuwa na uzalendo.
========
========

1 comment:

  1. Huo ndo ushabiki wa kijinga, huvi Malinzi ndo kaonewa tu?

    ReplyDelete