Search This Blog

Saturday, February 16, 2013

MSIMU WA VALENTINE NA BAILEYS WAFIKA TAMATI KWA MAFANIKIO

Miss Tanzania 2007 Richa Adhia aliyeshika chupa ya Baileys akiwa na
Gipson Godwin(kulia) na Scolastica Dotto ambaao ni mabalozi wa kinywaji
hicho kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti.


Miss Tanzania 2007 Richa Adhia  amewataka watanzania kujenga utamaduni wa kuwakupenda  na kuwajali watu wengine wakiwemo wenye mahitaji maalum kama watoto na wazee  kwa kuwa wanahitaji faraja toka kwa jamii nzima nyakati zote badala ya kusubiri  maadhimisho ya sikukuu mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kilele cha msimu wa  siku ya wapenda nao ulioandalia na Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji cha Baileys katika viwanja vya shoppers jijini Dar es Salaam,  Richa alisema “siku ya wapendanao ikitumika  kuongeza ari ya kuwasaidia watu wenye mahitaji inakuwa na maana zaidi kuliko kuitumia siku  hiyo kwa mapenzi zaidi na sio vibaya kutumia siku ya wapendanao  kuanzisha mapenzi mapya au kuboresha mapenzi yaliyokuwepo lakini pia itumike kuwakumbuka wahitaji ambao ni wazee na watoto”.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa vinywaji vikali kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti Emilian Rwejuna amesema “ tumeamua kufanya kampeni hii ili kuamsha ari ya kuwajali na kuwapenda wengine ikiwemo kujenga utamaduni wa kuwanunulia zawadi kama tulivyofanya kwa wapenzi wa kinywaji cha Baileys na kwa kuwa zawadi zina mchango mkubwa katika maisha ya mahusiano hivyo mtoto anayempa zawadi mzazi wake hujiweka katika mazingira mazuri kimahusiano kuliko asiyefanya hivyo”.Pia alielezea kuwa Kampuni ya bia ya Serengeti imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhamasisha na kutoa chachu na kuahidi itaendelea kuhamasisha mahusiano mema  miongoni mwa jamii.

Kampeni ya msimu wa valentine  iliyoandaliwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Baileys ilinza tarehe mosi mwenzi wa Februari kwa kupita katika maeneo mbalimbali ya manunuzi ili kuwahamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kuwanunulia wenzi wao zawadi na kukamalika siku ya wapendanao Februari 14. Ambapo zawadi mbali mbali zilitolewa katika kampeni hiyo ikiwemo chupa ya Baileys, fulana, glasi, maua na kubwa zaidi pea nane zilipata bahati ya kupata chakula jioni katika mgahawa wa Akemi uliopo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment