Search This Blog

Saturday, February 16, 2013

LIVE MATCH CENTRE: AZAM FC 3-1 AL NASIR



Dk 90+4 Gooo....! Tchetche anaipatia Azam bao la tatu akimalizia pasi ya John Bocco. Azam 3-1 Al Nasir.

Dk 87 Azam imebadilika inacheza soka la kasi sana na wanafika langoni kwa Al Nasir mara kwa mara.

Dk 80 Gooo....! Kipre Tchetche anaipatia Azam bao la pili kwa kichwa akimalizia krosi ya Khamis Mcha. Azam 2-1 Al Nasir

Dk 79 Al Nasir inafanya mabadiliko, ametoka Abdallmelik Sebit ameingia Emmanuel Manasi.

Dk 77 Timu zinashambuliana kwa zamu mpira umechangamka.

Dk 62 Azam inafanya mabadiliko, ametoka Abdi Kasim ameingia John Bocco.

>Dk 60 Al Nasir inafanya mabadiliko, ametoka Johnson James ameingia Adnan Nan.

Dk 57 Jabir Aziz wa Azam anakosa bao la wazi akiwa amebaki na lango la Al Nasir

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA!

Dk 45 HALF TIME!

Dk 44 Mpira umebadilika timu zinashambuliana kwa zamu sasa, Al Nasir wamezinduka.

Dk 38 Gooo....! Fobian Elias anaipatia Al Nasir bao la kusawazisha akimalizia pasi ya Kon James. Azam 1-1 Al Nasir

Dk 35 Azam inafanya mabadiliko, ametoka Bolou Kipre ameingia Jabir Aziz.

Dk 26 Timu zinashambuliana kwa zamu, Al Nasir japokuwa hawajapata bao lakini wanaonekana wana malengo.

Dk 16 Azam inafanya mabadiliko, ametoka Brian Umony ameingia Khamis Mcha.

Dk 14 Gooo...! Abdi Kasim anaipatia Azam bao la kwanza kwa kichwa akiunga krosi ya Kipre Tcheche. Azam 1-0 Al Nasir.

Dk 12 Timu zinashambuliana kwa zamu, Al Nasir wanacheza pasi nyingi.

Mpira umeanza hapa uwanja wa taifa

2 comments:

  1. tupia na picha za mabao au hata wanashangilia inaongeza mzuka huku kwa sisi tunaofatilia kwa website

    ReplyDelete
  2. Well done azam nawaombea simba nao kesho waweze kututoa kimasomaso

    ReplyDelete