Search This Blog

Friday, February 15, 2013

MARADONA APATA MTOTO MWINGINE AKIWA NA UMRI WA MIAKA 52

Diego Maradona amekuwa baba tena baada ya mkewe Veronica Ojeda kujifungua mtoto wa kiume ambaye amepewa jina la Diego Fernando Maradona Ojeda. 
 
Jorge Auruccio, mwanasheria wa Ojeda, alisema kwamba mtoto alizaliwa na uzito wa 3.2 kilograms (7 pounds) na alizaliwa jumatano saaa 11:57 p.m. kwa muda wa Argentina katika hospitali ya Buenos Aires. Alisema na mtoto na mama yake wapo kwenye hali znuri ya kiafya. 

Maradona mwenye miaka 52 tayari ana watoto wawili wa kike kutoka kwenye ndoa yake na Claudia Vallafane - watoto hao ni Dalma and Giannina. Pia mkongwe huyo wa soka ana watoto wengine wawili ambao amekataa kuwatambua - japokuwa vipimo vya DNA vilivonyesha ni baba wa watoto hao.

Auruccio alisema kwamba Maradona alikuwa Dubai lakini alikuwa anajua kila kitu kilichokuwa kinaendelea kuwa kujifungua kwa mwenza wake. 

Maradona pia ana mtoto mwingine wa kiume aitwaye Diego Armando Maradona Sinagra, ambaye alimzaa wakati akiwa nchini Italy akiichezea Napoli. 

"Jaji ameniamuru nimlee mtoto, lakini hilo halinifanyi nijihisi kumpenda huyo mtoto," alisema Maradona mwaka 2005. 

No comments:

Post a Comment