Search This Blog

Friday, February 15, 2013

BAADA YA KUTEMWA SIMBA - DANNY MRWANDA APATA TIMU TENA VETNAM

Miezi kadhaa baada ya kutemwa na klabu bingwa ya Tanzania bara, Simba Sports Club, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Danny Mrwanda sasa amepata timu ya kuichezea huko nchini Vetnam.

Mrwanda ambaye miaka kadhaa iliyopita alikuwa mchezaji tegemeo wa Simba kabla hajauzwa kwenda nchini Vetnam kucheza soka la kulipwa katika vilabu vya Dong Tam Long An na Hoang Anh Gia Lai na baada ya kumaliza mkataba wake akarudi bongo kujiunga na Simba, lakini muda mfupi baada ya kujiunga na timu akatemwa kwa madai kwamba kiwango chake kimeshuka

Akizungumza na mtandao huu Mrwanda amesema kwamba baada ya kuondoka Bongo, alirudi nchini Vetnam ambapo sasa ameweza kujiunga na mabingwa wa ligi kuu ya Vetnam klabu ya DA NANG FC kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.

"Nimepata timu huku ya DA NANG FC, hii timu ndio bingwa wa ligi kuu ya Vetnam. Sasa tutashiriki ligi ya mabingwa wa bara la Asia." - Alisema Mrwanda.

1 comment: