Search This Blog

Friday, February 15, 2013

BOCCO ARUDI DIMBANI, ANAWEZA KUANZA KESHO DHIDI YA WASUDANI - HUKU KOCHA STEWART HALL AKITAMBA KUSHINDA

AZAM FC inashuka dimbani kesho kuumana na Al Nasir ya Sudan Kusini katika pambano la raundi ya kwanza ya Michuano ya Kombe la

Shirikisho litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Azam inayoshiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu ilipotinga ligi kuu mwaka 2007, inalazimika kushinda mchezo huu na kujiweka katika nafasi nzuri yakusonga mbele.

Kocha wa Azam, Stewart Hall ametamba kuwa kikosi chake kipo tayari kwa mpambano huo kuhakikisha kinazindua kampeni yake kwa ushindi.

"Tumefanya maandalizi ya kutosha, tumecheza mechi nyingi za kujipima nguvu katika ziara yetu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Kenya sasa ni wakati wa kuwapa raha Watanzania kwa kuibuka na ushindi,".alisema Hall.

Katika pambano hilo,Hall huenda akampa nafasi japo kwa dakika chache  mshambuliaji John Bocco ambaye  afya yake imethibitishwa na daktari wa timu hiyo Mwanandi Mwankemwa kuwa imeimarika.

Bocco ambaye kwa muda mrefu amekuwa mpachikaji mabao tegemeo wa muda wote wa kikosi cha Azam alikuwa nje ya dimba kwa takribani mwezi mmoja baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.

Mwingereza huyo pia atamtegemea mshambuliaji mwingine tegemeo wa timu hiyo Kipre Tchetche kusaka mabao lakini ambaye atakuwa akilishwa mipira na Humprey Mieno, huku beki Jockins Atudo akisubiri kuzamisha mipira wavuni kwa mipira ya kona.

Pambano la marudiano kati ya Azam na Al Nasir litapigwa kati ya Machi 1,2 na 3 katika mji wa Juba,Sudan Kusini.

1 comment:

  1. god help azam am not azam fan but am tanzanian so go azam go

    ReplyDelete