Search This Blog

Sunday, December 9, 2012

YEW BERKO AENDA KUJIUNGA NA FC LUPOPO LEO ASUBUHI

Hatimaye leo majira ya saa moja asubuhi golikipa Mghana Yew Berko ameenda nchini Kongo kwenda kujiunga na timu ya FC Lupopo kwa mkopo akitokea Dar Young African.

Berko ambaye alijiunga na Yanga takribani misimu mitatu iliyopita amepelekwa Lupopo baada ya kukosa nafasi ya kudumu ndani ya kikosi cha Yanga mbele ya golikipa Ally Mustapha Barthez. Hivyo ikaamuriwa bora aende kwa mkopo Lupopo ambao walikuwa wakimhitaji kwa muda mrefu na nafasi yake imechukuliwa na Kabange Twite ambaye ni kaka yake na Mbuyu Twite wa Yanga.

"Ni kweli leo asubuhi Yew Berko ameondoka kwenda Congo kujiunga na FC Lupopo, ameondoka hapa kwa ndege ya shirika la Kenya Airways." kilisema chanzo cha habari kutoka Yanga.

2 comments:

  1. thats the best idea for yanga
    1.-alishaanza kuchoka na kuchemsha
    2.-alikua majeruhi wa bega mara kwa mara
    3.-anatoa nafas kwa makipa wazuri wa kibongo kama said mohamed kuonesha uwezo wao
    4.-yanga bado ina kipa bora tanzania kado alie kwa mkopo mtibwa
    5.-YAO NI KIPA WA UKWELI ALIEDAKA TZ MIAKA YA SASA

    ReplyDelete
  2. Siasa za viongozi wetu zimechukua nafasi yake kama kawaida yao,wahenga wanasema ukitaka kumuua paka basi mpe jina baya,,hakuna mtu kwenye nafasi yake hapa bongo mwenye uwezo km wake,.Makipa wa bongo wanapaswa wasikitike hasa wa Yanga,cz wao wangeweza kumtumia na kujifunza vitu vingi sana kutoka kwake,,ila siasa zinaua maendeleo ya mpira,.Haya yote yamefanyika ili kumridhisha Mbuyu twite,eti hajawahi kucheza tofauti na pacha wake,ndizo siasa za viongozi wetu,wanamridhisha mtu mmoja wa kuuwa watu10..Hata ujio wa kabange,kuna wabongo wenzetu nao watatafutiwa majina mabaya ili waondoke,,na ndio maana tunaambiwa mara bega,mara kiwango kimeshuka,mara anadharau,,sasa cha ajabu ikiuliza mlikaa nae muda gani,utasikia misimu mitatu,kwq huko nyuma hakuwa hivyo,?Au ndio paka anataka kuuliwa,,wachezaji waliobaki wajifunze kwa hili,km kaweza kuondoka berko mtu aliyeonekana tiba kwa Yanga,tena kwa kiwango cha juu,basi hata wale waliopo pia wataondoka km alivyoondoka mwezao,,Ila inawezekana kuna kipengele ktk mkataba wa twite kinachoonesha lazma pacha wake aje,,Kwa kuwa siasa ndizo zilichukua nafasi kuliko ueledi,basi hatunahaja kuheshimu maamuzi yao kwa faida yao na wala c faida ya klabu yao..NIYONZIMA AJIFUNZE KUPITIA KWA BERKO..

    ReplyDelete