Zikiwa zimepita siku kadhaa za mazungumzo juu ya kuongezwa kwa muda wa mkataba kiungo mshambuliaji wa Dar Young African - Haruna Niyonzima, hatimaye siku ya jana klabu bingwa ya Afrika mashariki na kati imefanikiwa kukubaliana kimsingi na mchezaji huyo kumuongezea mkataba mpya.
Taarifa rasmi nilizozipata ni kwamba Haruna Niyonzima ambaye amebakiza miezi sita katika mkataba wake na Yanga amekubali kuongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga.
"Niyonzima alikuja Tanzania siku tatu zilizopita kwa ajili ya mazungumzo na uongozi wa Yanga, lakini mwanzoni hawakupata muafaka, ila hatimaye jana alikubaliana na Yanga kuongeza mkataba wa miaka miwili kwa kulipwa dola 70,000 kama fedha ya usajili na mshahara wa dola 3,000 kwa mwezi," kilisema chanzo cha habari kilicho karibu na uongozi wa Yanga.
jamaa amenogewa ela ndogo kwao ndio maana wengi wanakimbilia tzn,ila nashangaa watanzania wanashindwa kujituma kama wageni.
ReplyDeleteMATAJIRI WA BONGO WANATOA PESA NYINGI SANA KWA WANASOKA WA NJE WAKATI WENGINE VIWANGO VYAO SAWA NA VYA WA HUMU, WABONGO WAKAZE MSULI NAO WAPATE NAFASI KUBWAV KATIKA SOKA LA NJE, TUJIFUNZE KWA WENZETU.
ReplyDeletekaona inalipa,yanga wanamwagiwa manoti tele,mungu ibariki dar young africans,niyonzima kaza msuli,
ReplyDeleteKwa mtazamo wa haraka na wa kinazi tutampongeza Haruna,lkn kimaendeleo ya soka basi kachemsha,nilimsikia kwenye chombo kimoja cha habari,,namnukuu..Alisema hawezi kucheza soka ndani ya Afrika zaidi zaidi ya Yanga,kwa sababu hakuna mabadiliko,akitoka Yanga tu safari ni nje ya Afrika,kauli hii aliitoa pale aliposikia Elmerekh wanamtaka,Lakini ni kitu ambacho si kweli,,kwa timu km Elmerekh yenye mafanikio Afrika,angeweza kuboresha kiwango na kujifunza zaidi kwa sababu kule anakutana na wachezaji wengi wenye kaliba km yake,,lkn c ligi yetu,miezi3 inachezwa na miezi5 inasimama,huwezi kuwa bora,.kwa viongozi wa Yanga nawapongeza kwa kumbakisha kwa sababu wanalinda maslahi yao na wala c ya mchezaji,kumfanya mjinga na hadi kusaini na kuona Yanga ni sawa na Elmerekh,hata km viongozi wa Yanga waliweka dau kubwa,kwa kuzingatia mkataba wa haruna ulibaki miezi6,basi alikuwa na uwezo wa ushawishi wa kutaka kuondoka..Ila kwa kuwa bongo anaishi kifalme,maisha yanataka nini tena,asubiri tu azoeleke kisha aambiwe kiwango kimeshuka,azomewe na auzwe kwa pesa ya madafu tena c tu ndani ya Afrika,bali ndani ya A.Mashariki..
ReplyDelete