Kocha mpya wa timu ya taifa ya Brazil Luis Felipe Scolari amesema anaamini kwamba kocha wa timu ya Real Madrid na nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo wanastahili kutwaa tuzo za kocha na mchezaji bora wa dunia mwaka huu.
Akizungumza na mtandao wa FIFA, Scolari ambaye amewahi kuwa kocha wa Ronaldo alipokuwa mwalimu wa Ureno amekaririwa akisema kwamba Cristiano amekuwa kwenye kiwango bora kwa takribani miaka 5 sasa na ameshinda Ballon d'Or mara moja tu.
"Nimewaona Messi, Iniesta, na Ronaldo wakicheza lakini nimefanya kazi na Cristiano tu. Nafikiri anastahili kupata tuzo hiyo, kwa sababu amekuwa bora kwa miaka mingi sasa akiwa na United, Ureno na Real Madrid. Ningempigia kura ashinde. Pamoja na kipaji alichonacho, nafahamu namna anavyojituma na anavyoipenda kazi yake - nafikiri ni mchezaji bora duniani."
Alipoulizwa juu ya nani anastahili kuwa kocha bora wa dunia kati ya Jose Mourinho, Guardiola na Vicente Del Bosque, "Ningemchagua Jose Mourinho, kwa sababu nafikiri ni mmoja wa makocha bora na amekuwa anafanya kazi nzuri tangu alipokuwa FC Porto, then akaenda Chelsea, Inter Milan na sasa Real Madrid. Hivyo Mourinho ni bora kwa upande wangu."

No comments:
Post a Comment