Search This Blog

Wednesday, December 19, 2012

MANCHESTER UNITED NA SAKATA LA KUBEBWA



MIMI  AMBAYE NI MDAU WA  SPORTS EXTRA  NAPENDA  KUONGELEA  KAWAIDA  ILIYOPO  KWA  MASHABIKI  WENGI  WASIOIPENDA  UNITED  AMBAO MARA NYNGI WAMEKUWA WAKISEMA  INABEBWA,  KWA  UJUMLA  SUALA  HILI  MARA  NYINGI  HUA  NALICHUKULIA  KISHABIKI  JAPO  KUWA  HUWA  NAONA  WAO WAPO  SERIOUS.
LAKINI  KUBWA ZAIDI  WATANGAZAJI  NAO  WAMEKUA  WAKIWAUNGA  MKONO  MASHABIKI  HAO NA  HASA  WATANGAZAJI  WA  SPORTS  EXTRA  HUWA  NAWASIKIA  MARA  KWA  MARA PAMOJA NA KATIKA  SPORTS  BAR (Labda pia ni kwasababu ndio kipindi cha michezo cha redio na TV ambacho huwa nasikiliza hivyo sijui redio na TV zingine kama nao hua wanaiponda man united).
SASA HILI  LA  WATANGAZAJI  NDIO  LIMENIFANYA  NIANDIKE  WARAKA  HUU  SABABU  NYIE  NDIO  TUNAWATEGEMEA  ZAIDI  KUTUPA  ELIMU/TAARIFA  ZA  KIMICHEZO  NA  BURUDANI  KWA USAHIHI.
NILITEGEMEA  MNGEENDELEA  KUWA  TETRACICLINE  HATA  KATIKA  ANGA  ZA  KIMATAIFA  KAMA  ILIVYO  HAPA BONGO,  JAPO  KUNA  BAADHI  YA  MASHABIKI  WA  HAPA  BONGO  UPANDE  WA  MSIMBAZI  WANAWASAKAMA NYIE  HASA  SHAFII  KWAMBA  ANAFAGILIA  JANGWANI,  HAPO NAWEZA  KUWASHANGAA HAWA  MASHABIKI  KWA   KUSAHAU  KUWA  KUNA  WAKATI  HUKOHUKO  JANGWANI  SHAFII  ALISHAZUSHIWA  KUWA  ANATUMA E-MAIL  KWA  MAXIMO  ILI  MAXIMO  ASIJE  YANGA. KWAKWELI KWA HAPA BONGO NAWASIFU KWA KUWABANA WABABAISHAJI WA MPIRA  WA  BONGO  MKO  JUU NA  HAMUONYESHI  MAHABA  KWA  UPANDE  WOWOTE.
TUKIRUDI KWENYE  MADA  KUU   UNITED  KUBEBWA  NDANI  YA  EPL    
HIVI  SASA  IMEKUWA  NI  KAWAIDA  KILA  MAN UNITED  ANAPOPATA  FAIDA  KWA  MAKOSA  YA  REFA  INAONEKENA  MAN  U  KABEBWA  NA  SIO  KOSA  LA  MWAMUZI  LAKINI  MWAMUZI  HUYOHUYO  ANAPOIUMIZA  MAN  U  INAKUA  NI  KOSA  LA  MWAMUZI  NA  SIO  KWAMBA  MPINZANI  AMEBEBWA  SASA  NASHINDWA  KUELEWA  HII  TERMINOLOGY  YA  KUBEBWA  TAFSIRI  YAKE  NI  NINI?.
KUNA  MIFANO  MINGI  AMBAYO  INAONYESHA  NAMNA  AMBAVYO  UNITED  IMEKANDAMIZWA  NA  WAAMUZI  NA  MIFANO  MINGI  AMBAYO  TIMU  ZINGINE  ZIMEFAIDI  DHIDI  YA  UNITED  NA  PIA  DHIDI  YA  TIMU  ZINGINE;
1.     KOLO TOURE  ALISHAWAHI  KUDAKA  SHUTI  LA  ROONEY  NDANI  YA  MITA  6 WAKATI  KIPA  ALISHAPOTEA  NA  REFA  HAKUONA  TUKIO  HILO  UNITED  WAKAPEWA  KONA  BADALA  YA PENALT- hakuna  aliyeshika  bango
2.     FLETCHER AKIWA KTK KIWANGO BORA  ALIIKOSA  FAINALI  YA  BARCELONA  MWAKA 2009  BAADA  YA  KUPEWA  KADI  NYEKUNDU  ISIYO  SAHIHI NA PENALTI  IKAPIGWA  KTK  NUSU  FAINALI- hakuna  aliyeshika  bango
3.     DROGBA  ALISHAFUNGA  MAGOLI  YA OFF SIDE  MFANO DHIDI  YA  MAN CITY  NA  PIA DHIDI YA  MAN  UNITED  MWAKA 2009 NA  CHELSEA  WAKACHUKUA  UBINGWA  KWA POINT  MOJA  JUU YA UNITED.  hakuna  aliyeshika  bango
4.     DEMBA BA WA NEWCASTTLE  ALIZAWADIWA PENALT 28/11/2011 WAKATI  RIO  RERDINAND  HAKUCHEZA  FAULO.  hakuna  aliyeshika  bango
5.     JUZI 9/12/2012 GOLI  LA  ASHLEY YOUNG  LIMEKATALIWA  DHIDI  YA MAN CITY.  kuna  mashabiki  mpaka  leo  wanasema  Young  alikua  offside.   ILA HILI  CLOUDS  WALIZUNGUMZIA  NA  HATA  SHAFII  AME-POST  KTK  BLOG  YAKE  KUONYESHA  KUWA  YOUNG  HAKUWA  OFFSIDE  ILA  ALICHOMOZA  WAKATI  WA  KUICHEZA  RE-BOUND AMBAPO  HAPO  HAKUNA  OFFSIDE
6.     JUZI  9/12/2012  PIA  EVRA  ALINYIMWA  PENALT  KWA  FAULO  YA  KOLO  TOURE  NDANI  YA MITA  18.  hakuna  aliyeshika  bango
7.     SANT CARZOLA ALIPATA PENALT ISIYO SAHIHI DHIDI YA WEST BROM  MPAKA  KOCHA  WAKE  KAOMBA  MSAMAHA.  Angalau Wenger kaonyesha uanamichezo
8.     MATERSAKA  ALISHIKA  MPIRA  NDANI  YA  MITA 18  LAKINI  WEST BROM  HAWAKUPEWA  PENALT  WAKATI  ARSENAL  WALIPATA  PENALT  MBILI  KATIKA  MECHI  HIYO.  hakuna  aliyeshika  bango

KUTOKANA  NA  MIFANO  HIYO  MICHACHE  SIJAWAHI  KUSIKIA  MASHABIKI  AU  WATANGAZAJI  WAKISEMA  ARSENAL  AU  CHELSEA  AU  MAN CITY  KABEBWA  AU KUSIKIA  KUWA  DROGBA NI  MUOTEAJI, ILA  UTASIKIA  ‘’MAKOSA  YA  REFA’’  ‘’REFA NAE  BINADAMU’’  AU  PRESHA  ILIKUA  KUBWA  HIVYO  REFA HAKUONA.  LAKINI  KWA UNITED SABABU HUWA  SIO  PRESHA, NA  HAPO  INASAHAULIKA KABISA  KUWA  KARIBU  MECHI  ZOTE  ZA  UNITED  HUWA  PRESHA  YA  MCHEZO  IKO  JUU.

KWA  MTAZAMO WANGU;
 UNITED  INACHUKIWA  NA  WENGI  SABABU  YA  MAFANIKIO  YAKE.  NDIO  MAANA  HATA IKIFANYA  VIZURI  WATU WANATAFUTA WAPI PA KUSHIKA KAMA WAFA MAJI, KUNA KIPINDI KIKOSI  KILIKUA KINATISHA SANA  KILIKUA  KINAPIGA GOLI NYINGI KILA MPINZANI  PALE ENGLAND  BASI  WAPINZANI  UTETEZI  WAO  IKAWA  ‘’UNAMKUMBUKA  REDONDO?’’  ‘’UNAMKUMBUKA  KAKA?’’,  ‘’KIBOKO  YENU  MADRID’’  BADALA YA KUONGELEA  TIMU ZAO.  KWASASA  TIMU  INASHINDA  JAPO  HAITISHI  SANA,  SASA WANASEMA ‘’INABEBWA’’. KIFUPI  HAWAKUBALI  UKWELI  SUALA  AMBALO  SIO  UANAMICHEZO.  MCHEZAJI  AKIWA  UNITED  SIO MZURI  AKITOKA  ANAKUA  MZURI  KWA  KIWANGO KILEKILE  MFANO  MZURI NI  RONALDO  NA SASA  VAN  PERSE  ONA HATA  KWASASA  YALE  MAJINA HATUYASIKII  TENA  ‘’VAN MAGOLI’’  ‘’VAN   HAKUNAGA’’  YAMEISHIA WAPI NA KIDUME BADO ANATUPIA!  KAZIPIGA TIMU  KUBWA ZOTE MPAKA SASA.
KAKA  SHAFII  ALIKUWA NI MTU AMBAYE  ANAMFAGILIA  SANA  RVP  NA  KUMPAMBA KWA MAJINA  HAYO LAKINI  KWA SASA  KAHAMIA  KWA  FALCAO.
SIJUI  ITAKUAJE  PALE  RVP  ATAKAPOKUJA  KUWA  KAMA  TORRES  ALIVYO  SASA 
AU  SIJUI  ITAKUA  VIPI  IKITOKEA  GHAFLA  JANUARY  FALCAO  AKATUA  MAN UNITED.

UNITED INA MASHABIKI WENGI LAKINI PIA INA WAPINZANI WENGI;
SABABU WALE  WOTE  AMBAO  HUWA INAPAMBANA  NAO NA BAADAE  WAKAKATA  PUMZI WENGI WAO HUANGUKIA  KWA WAPINZANI WENGINE, MFANO MZURI  TANGU 1992 NDANI YA PREMIER LEAGUE UNITED IMEBADILI WAPINZANI WENGI. BINAFSI  NIMEANZA  KUFUATILIA KIDOGO LIGI HII MWAKA 1996 NA NIKAWA ZAIDI MWAKA 1998 MPAKA SASA.
HIVYO  KUMBUKA  KUWA  TANGU 1992 WALIKUWEPO  LIVERPOOL,  LEEDS UNITED (Kina Tonny Yeboah), BLACKBURN ROVERSE (Kina Allan Wright na Allan Shearer kabla hajaingia Newcastle mwaka 1996 kwa £15 million) , NEWCASTLE UNITED (Kina Les Ferdinand na Faustin Asprilla)  WAKAJA ARSENAL   WAKAJA CHELSEA (miaka ya 2000 baada ya kuja Abramovich) WAKAJA MAN CITY (baada ya sheikh Mansoor)
HAWA NINAOSEMA  WALIKUJA  SINA MAANA KUWA  HAWAKUWEPO  AU KWAMBA  NAWADHARAU  ILA  NI KWAMBA  WALIKUA KAMA  ASTON VILLA WASASA (yaani walikua wa kawaida tu). HII  NI DHAHIRI KUWA WALE WALIOKUA  LEEDS, NEWCASTLE NA BLACK BURN+ WALE WASIOZIJUA HIZO TIMU KAMA LEEDS  NDIO  SASA  WAKO  KWA  MAN  CITY  NA CHELSEA. NA  PIA  WAKIKIMBIA  LIVERPOOL  NA  ARSENAL  WENGI  WANAENDA HUKO(CITY NA CHELSEA).  HIVYO CHUKULIA  HAO  TU WALIOKUA TIMU  HIZO SABA WAWE DHIDI YA  UNITED  INAKUAJE  HAPO  HALI  YA  HEWA  LAZIMA  ICHAFUKE,  ACHILIA  MBALI  TIMU  ZINGINE  ZOTE  ZINAZOSHIRIKI  LIGI  KUU.

SABABU  YA  KUSEMA  TIMU HIZI  ZINAIKIMBIZA  UNITED  NI  KUWA  TANGU  1992  UNITED  INABADILISHA  WAPINZANI  WA  MBIO  ZA  UBINGWA  SABABU  IMEKUA  AKIKOSA  UBINGWA ANAKUA  WAPILI  ISIPOKUWA  MISIMU  MITATU TU (2001/2002, 2003/2004 NA 2004/2005 TU) INAMAANA HII MISIMU MITATU NDIO  ALIFANYA  VIBAYA  ZAIDI  NA  HAPA  TATIZO  KUBWA  ILIKUA  PENGO  LA  PETER  SCHMEICHEL KABLA YA KUPATA KIPA MWINGINE  MZURI,  JE  HII INAWEZEKANA  KWA  KUBEBWA  TU!?.  HAO  WABEBAJI  HAWACHOKI  KATIKA  MIAKA  YOTE  HIYO?.
 WAKATI HAWA WENYE UWEZO KAMA  LIVERPOOL  AMESHAWAHI  KUWA  WA  8 MWAKA 1993/94 NA  ARSENAL  AMESHAWAHI KUWA WA 12 MWAKA 1992  SIKUAMBII KUHUSU  CHELSEA  NA  MAN CITY.

MSAADA

IKIWEZEKANA  TUSAIDIANE  ILI  KAMA NI KWELI  TUWEZE  KUJUA   UNITED   ANATOA  NINI  ILI  KUBEBWA  AMBACHO  KINAWASHINDA   MAN  CITY, CHELSEA  AU QUEENS PARK RANGERS KUTOA  ILI  NAO WABEBWE!?

UNITED  NDANI  YA  CHAMPIONS  LEAGUE

UNITED HUYU  ANAYEBEBWA  KWENYE EPL  VIPI  KWENYE  CHAMPIONS  LEAGUE MBONA  NI BINGWA  MARA  3  NA KACHEZA  FAINALI  NYINGI TU NA ALISHAKUA BINGWA WA VILABU DUNIANI.  VIPI  HAWA  WENYE  UWEZO  WA MPIRA KAMA  ARSENAL, MAN CITY  MBONA  HATA  KOMBE HAWAJAWAHI  KUBEBA,  NA  CHAMPIONS  LEAGUE  INACHEZESHWA  NA  MAREFA  WENGI  WA  KIWANGO  CHA  JUU  WASIOTOKA  UINGEREZA KWENYE MAREFA WACHOVU KAMA WAO WASEMAVYO?.


NAOMBA  MUELEWE  KUWA  MPINZANI WA  UNITED  HAWEZI  KUISIFU  UNITED
·       HATA  MOURINHO  ALIPOKUA  CHELSEA ALIKUWA  ANAMPONDA  RONALDO  NA KUMUITA  MSHENZI  HANA  ELIMU, LAKINI  KWASASA  NDIE  ANAYEMPA  UHAKIKA  WA  KULA  FEDHA  ZA PALE SANTIAGO BERNABEU  (sio siri ndio jembe lake) NA UTAMWAMBIA  NINI KUHUSU  RONALDO.


MTANGAZAJI  ANAYEONGOZA  KWA  KULIPEPERUSHA  NENO  MBELEKO  KWA  UNITED 
NI  ALEX  LUAMBANO  SABABU  HATA  IKISHINDA  BILA  REFA  KUIPA  FAIDA  YEYE  ATAULIZA  MBELEKO  VIPI.  MFANO  KUNA  SIKU  ALIKUA  YEYE  NA  JEFF REDIONI  UNITED  ILIKUA  IMEPATA  MATOKEO  MAZURI  KTK  MECHI  KUBWA  AMBAYO SIKUMBUKI VIZURI  ILIKUA  KAMA  SIO  DHIDI  YA  ARSENAL  BASI  NI  LIVERPOOL  AU  CHELSEA  NDANI  YA  MSIMU  HUU.  JEFF  AKAWA  ANASEMA  UNITED  WANGETULIA  WANGEPATA  MAGOLI  MENGI  LAKINI  LUAMBANO   AKAWA  ANACHOMEKEA  MANENO  YANAYOMAANISHA  MBELEKO  ILIISHIA  HAPO  NDIO  MAANA  HAWAKUFUNGA  ZAIDI.
VITU  KAMA  HIVI  SIDHANI  KAMA  NI  SAHIHI  KWA NYIE  WATANGAZAJI  KUVIONGEA  HEWANI  SABABU  NI  DALILI  YA  KUONYESHA  MAHABA  YENU  KWA  HIZI  TIMU  HALI  YA  KUWA  MNATAKIWA  KUWA  NEUTRAL  PINDI  MUWAPO  HEWANI.

HAIWEZI  KUWA  RAHISI  KUWABADILI  MASHABIKI WOTE  HUKU  MTAANI  SABABU  WAKO  HURU  KUONGEA  CHOCHOTE  JAPO  WENGINE  HATA  HIZO  MECHI  HUA  HAWAANGALII  ILA  WANAONGEA  TU.

USHAURI  WANGU
·      NI  KAMA  NI  LAZIMA NENO KUBEBWA  LITUMIKE HEWANI  BASI  LITUMIKE  KWA  USAWA  PALE  MWAMUZI  ATAKAPOIPA  FAIDA  TIMU  YOYOTE BASI IWE  HIVYO  KUWA  TIMU  ILE  IMEBEBWA  NA  SIO  NENO  HILO  KUAMBATANISHWA  NA  UNITED  TU HIYO  ITAKUA SIO  FAIR.
·      WATANGAZAJI  MUWAPO  HEWANI  HAMTAKIWI  KUONYESHA  MAPENZI  YENU  KTK  TIMU YOYOTE. NA HATA UKIONYESHA KUIPONDA SANA  TIMU  FULANI WAKATI  INAFANYA VIBAYA  KUWA  TAYARI  KUISIFIA SANA  INAPOFANYA  VIZURI  KINYUME NA  HAPO  ITAKUA  NI KAMA  WEWE  UNAOMBEA IWE INAFANYA  VIBAYA  TU  ILI  UPATE CHA  KUONGEA (Yaani usiwe na uchambuzi wa kina ktk mabaya tu wakati yanapokuja mazuri ya timu hiyo unaona ni kitu cha kawaida tu, na ku-act kuwa hauko deep kwenye mambo mazuri ya timu hiyo ‘’that is not fair’’) FAIR PLAY SIO KTK PITCH PEKEE NI HATA HUKU KWENYE HABARI.    
·      NA  KUWA TUJARIBU  KUUPA  SUPPORT  MSEMO  WA  JEFF  KUWA  TUNATAKIWA  KUWAPA  HESHIMA  ZAO  WAPINZANI  PALE  WANAPOPATA  USHINDI  KWA  JUHUDI  ZAO. NA NDIO  MAANA VYAMA VYA MICHEZO  HUMWAJIBISHA MWAMUZI PALE  ANAPOCHEMSHA NA SIO TIMU ILIYOPATA FAIDA KUTOKANA NA MAKOSA YA MUAMUZI.

NINA UHAKIKA KUWA HAYA YOTE NYIE WATANGAZAJI MNAYAFAHAMU ILA HII NI KUKUMBUSHANA TU NA KUCHANGIA MAWAZO ILI HATA WASIKILIZAJI WENGINE WAWEZE KUPATA KILE WASICHOFAHAMU.  
PIA MIMI KWA UJUMLA NAOMBA MUENDELEE KUTUPATIA HABARI SAHIHI KAMA MFANYAVYO SASA. SABABU MAMBO MENGI HUWA TUNAANZA KUYASIKIA KWENU NA BAADA YA MUDA TUNAYASHUHUDIA DHAHIRI.
HUO NI UTHIBITISHO KUWA CLOUDS NI CHOMBO AMBACHO KINA WAANDISHI MAKINI NA WATANGAZAJI BORA HAPA TANZANIA KUTOKANA NA KUA NA HABARI ZA UHAKIKA KILA WAKATI.

KWA LEO NI HAYO TU.
NATANGULIZA SHUKURANI ZANGU KWENU.
MDAU-SPORTS EXTRA






17 comments:

  1. Mie si shabiki wa man U ila napenda sana mafanikio ya timu hii pamoja na staili yao ya kucheza, pia mikakati yao. Kwa jinsi ulivyoeleza wapingao watapata faida ya kujua kile walichokuwa hawajui.

    ReplyDelete
  2. Eeh bwana umenikosha kwa kuongelea hili suala! Sie mashabiki wa Man U tunapata taabu sana kushangilia timu inapofanya vizuri kwa maneno ya hasa watoto wa Arsenal!

    ReplyDelete
  3. naona umepost usichokifahamu,sidhanikama unaweza kusema kuwa liverpool arsenal na timu zingine zilikuwa kama Aston villa kwa hiyo una maana ya kwamba manchester toka mwaka 1992 MPAKA 2000 ndo amechukua ubingwa EPL?KAMA Arsene wenger aliomba msamaha kwa kulitambua hilo je mbona furgerson cjawai kumskia wakati anapoona kabebwa?

    ReplyDelete
  4. kaka tunakushukuru sana, ila upo sahihi ingawa si sahihi zaidi fahamu ndani ya uingereza yenyewe natumai haujafika kule mashabiki wa timu zote zilizo bakia wanalalamika kuhusu kubebwa kwa man u. Hivyo usiwasakame waatangazaji waki bongo kwani wao wanaongea kutokana na hali halisi ya mechi mbona baadhi ya magoli na mechi mlizo bebwa huzitaji. Kaka jipange upya huo ndio mpira na hiyo ndio radha yake. Pamoko luambano karibu cfc

    ReplyDelete
  5. Kweli kaka penye ukweli uongo hujitenga,mashabiki wa bongo macho yao hayajui mpira unavyochezwa bali yanatazama kiushabiki. Hali hii mdau mwenzangu hata ukifuatilia mashabiki wa Simba na Yanga jicho halitazami kiufundi bali kishabiki,vile vile hata watangazaji wa vyombo vya habari hata waandishi wa magazeti ya michezo mfano DIMBA,CHAMPIONI,SPORTI STAREHE, NK huchambua jambo kiundani tena kishabiki kuizungumzia YANGA upande wa uzuri kwa mtazamo wao lakini ukifuatilia ukweli wa mambo ulivyo ni uzushi ushabiki ndio uliojaa. Jamani watanzania wenzangu tujirekebishe kwa hili linatutia aibu kubwa na kuonekana hatujui mpira. Wadau wenzangu tuna haja ya kumpongeza aliyeandika makala maana anatukumbusha kuwa tuliko tunaelekea KIBLA na inaonesha umbumbumbu juu ya mchezo wa mpira wa mpira wa miguu au pale UDSM maarufu kwa VILAZA. Ndugu zangu tubadilike. BY MKINGA MWL

    ReplyDelete
  6. ALEX LUAMBANO ANA UPEO MDOGO SANA WA KUFIKIRI,
    NDO MAANA HUWA HAONGEI POINT HATA SIKU 1.

    ReplyDelete
  7. HOJA YAKO HAINA MSINGI NAOMBA UFANYE KITU KIMOJA CHA MSINGI NDUGU YANGU CHUKUA KARATASI A4 MBILI MOJA ANDIKA MAKOSA AMBAYO TIMU PINZANI WAMEPENDELEWA NA MAREFA NA NYINGINE ANDIKA MAKOSA AMBAYO TIMU YAKO YA MAN U IMEPENDELEWA NA MAREFA!TANGIA UANZE KUJUA MPIRA UMEPATA MAKOSA 8 TU YA TIMU PINZANI KUPENDELEWA NA MAREFA ILA KWA MWAKA MSIMU HUU TU WA LIGI MAN U IMEBEBWA ZAIDI YA MARA 8!NAKUJA NA EVIDENCE SUBIRI USIWE MNAZI KAKA UKWELI UNAJULIKANA MAN U INABEBWA KUTOKANA NA UWEPO WA BABU PALE TRAFORD SUBIRI AKISTAAFU ZAMA ZITABADILIKA

    ReplyDelete
  8. Sioni cha kujadili hapa maadam umeshasema ni mambo ya ushabiki! mpira unachezwa na unachezeshwa na binadamu ambao wana mapungufu yao, na yote hayo kwa ujumla wake ndio yanayoleta ladha ya mchezo wenyewe. ingekuwa soka linachezwa/linachezeshwa na roboti sina hakika kama sote tungekuwa mashabiki!

    ReplyDelete
  9. Nadhani watakuwa wamekuelewa mdau wa sports extra,ingawa najua neno lako sio sheria.Umenena ukweli nami nakuunga mkono kwa hayo.

    ReplyDelete
  10. unafaa kuwa mtangazaji,kaka unaujua mpira, shukrani

    ReplyDelete
  11. NADHANI WEWE UMEZUNGUMZIA USHABIKI TUPU HAPO JUU WALA MIFANO YAKO HAINA HUUSIANO NA MAN U KUBEBWA ILA UKWELI NI KWAMBA MNABEBWA SANA MBONA UJAZUNGUMZIA RED CARD MBILI DHIDI YA CHELSEA?USILINGANISHE MAKOSA YA WENGINE NA MAN U NYIE NI KWA PERCENTAGE KUBWA ZAIDI NDO MAANA MNASEMWA DUNIA NZIA JAPO MAKOSA KWA MAREFA YANATOKEA KAMA BINADAMU MWINGINE. NDO MAANA KUNA TETESI KWAMBA DIRISHA DOGO MNASAJILI MAREFA WAKATI SISI TUNAANGAIKA NA WACHEZAJI.EMILY

    ReplyDelete
  12. WEWE UJAOWANISHA MATUKIO KWANINI MNABEBWA ILA UMEJARIBU KUONESHA MAKOSA YA TIME NYINGINE, REFA KAMA BINADAMU LAZMA HAWE NA MAKOSA ILA KWANINI YANAKUWA KWA MAN U PERCENTAGE KUBWA??? MBONA UJAONESHWA ULIVYOBEBWA HATA RED CARD MBILI DHIDI YA CHELSEA UJAZUNGUMZIA HAPO, ACHA USHABIKI BANA.
    EMILY

    ReplyDelete
  13. well umeandika ujumbe makini sana mwenye kuelewa ataelewa wewe umeongea nini na mwenye kujua atajua.

    ila linapokuja swala la watangazaji wa kitanzania hawana ethics za uandishi hata kidogo amini nachokwambia waandishi wachache sana wanajua wanafanya nini katika 10 basi 2 ndo wanajua ila waandishi wengi waliopo hapa tanzania kuanzia magazeti mpaka kwenye blog wanazomiliki ukifailia inaskitisha sana kiukweli,

    bro unaesema hata ulaya wanajua kuwa man u inabebwa sio kweli, ushawai kuwepo uko..? au unasema tu kwa kuwa wewe huipendi man u. watu wanaoichukia man u ndo wanafanya man u iwe klabui kubwa duniani ila me nawashangaa watanzania wengi wao wanakuwa ma judge wazuri wa kila kitu sisi ni third world coyuntry ambao hata mawazo yetu hayaendi kwa wahusika.

    once united always united haterzz ur making us famousssss

    ReplyDelete
  14. uko sawa kwa upande wamarefa wanapokosea ionekane wamekosea marefa na co team imebebwa,pia na sisi huligans tuwe fair kwa kila litupendezalo nakutukera toka kwa waandish wa habari za michezo,km umeweza kugundeua kua ALEX ANAIPONDA MAN pia utakua unajua kua SHAFFY NA GEF PIA NIWANAZI WA MAN U c walaumu kwakucfia ushind wa MAN U vs QPR nakuaxa kuxambua vizur mech ya SPURZ vs CHELSIE kisa CHELSIE ama Arsenal zimeshinda game zake,nao n binadam NDO MANA WENZAKO TUNAWAVUMILIA ILI TUZIDI KUPATA VINGI VYA MSINGI KULIKO MADAI YAKO NA RECORD ZAKO NYEPES.GLORY GLORY MAN U.

    ReplyDelete
  15. uwezi ukamwita jirani yako mwanaumeeee

    ReplyDelete
  16. MAN Utd kiboko yao BARCELONAAAAA.
    Wanabebwa,Wanabebwa,Wanabebwa,Wanabebwa,Wanabebwa,Wanabebwa,Wanabebwa,Wanabebwa,Wanabebwa,Wanabebwa,Wanabebwa,Wanabebwa,Wanabebwa,MAN UTD Wanabebwa,MAN UTD Wanabebwa,MAN UTD Wanabebwa,MAN UTD Wanabebwa,MPAKA MWISHO WA DUNIA

    ReplyDelete