Ngassa akisalimiana na Manji |
Ngassa ambaye alirejea Tanzania hivi karibuni akitokea nchini Rwanda alipoenda na timu ya Tanzania bara kushiriki michuano ya Kombe la CECAFA Challenge Cup amekuwa hapatikani kwenye simu zake za mkononi na wala kwake hayupo, jambo ambalo limewapa hofu viongozi wa Simba na Azam ambao tayari wameelewana na wanachosubiri ni kumpa taarifa mchezaji husika.
Kutokana na kupotea huko kwa Ngassa bila taarifa zimeibuka tetesi kwamba viongozi wa klabu yake ya zamani ya Yanga wamemteka wakijaribu kumshawishi akatae kujiunga na El Merreikh na arudi jangwani huku wakimuahidi mapato mazuri kama ilivyo kwa Haruna Niyonzima.
smba na yanga au simba na Azam?????
ReplyDeletemwandishi kuwa makini na unachokiandika basi, kwan unatuweka mguu upande baadala ya mguu sawa
ReplyDeletehuyu shafih dauda yanga imemkaa sana kichwani yaani mpaka anapoandika taarifa hizi ameisahau kabisa timu ya azam..?
ReplyDeletehata taaluma ya uandishi sijui hata kama anaijua, ukijaribu kufwatilia habar zake nyiingi ni za kukopi na kupesti, so km sorce yake ni uongo nae anaendeleza kulisha watu uongo, sijui kama anajua anachokifanya kwa kweli, jirekebishe kaka. blog yako imegeuka kuwa km magazeti ya udaku
ReplyDelete