Search This Blog

Friday, November 9, 2012

KUMUACHA AGGREY MORRIS KUNDINI KUTAIPELEKA AZAM KUBAYA

Siku mbili zilizopita klabu ya Azam FC ilifanya maamuzi magumu ya kuwasimamisha wachezaji wake watatu kati ya sita waliotuhumiwa kula njama na kupokea rushwa kutoka kwa vilabu vya kulwa na doto wa soka la Tanzania ili LambaLamba ifungwe na vigogo hao wa soka nchini.

Wachezaji wa Azam FC waliotuhumiwa na baadhi kukiri na kuchukua rushwa hiyo ni pamoja na Deo Munishi ‘Dida’ na mabeki Said Mourad na Erasto Nyoni ambao mpaka sasa wameshasimamishwa - huku nahodha Aggrey Morris ambaye nae ameshakiri kupokea mlungura akiachwa bila kuadhibiwa kwa sababu wanazozijua wenyewe Azam. Pia kuna wachezaji wengine wawili viungo wapo katika mkumbo huo lakini bado hawajatajwa.

Sasa ikiwa imepita siku moja baada ya kuibuka kwa mambo hayo ndani ya klabu ya Azam, kuna taarifa za kuaminika kwamba suala la kutoadhibiwa kwa nahodha Aggrey Morris ambaye ameshakiri kushiriki katika zoezi la upokeaji rushwa limeanza kuleta mgawanyiko mkubwa ndani ya kikosi cha Azam FC.

Ripoti kutoka ndani ya chanzo kilichopo karibu na kikosi cha timu hiyo kinasema kundi kubwa la wachezaji wa Azam wamechukizwa sana na kitendo walichofanya wenzao na wamefurahia kusimamishwa kwa Dida, Nyoni na Morad lakini bado wamekataa katukatu kuendelea kuongozwa na mchezaji ambaye amekiri kuchukua mlungura ili timu ifungwe au kucheza vibaya. Hivyo wanahitaji Aggrey Morris nae aadhibiwe na hata ikiwezekana kuporwa unahodha kwa sababu anakosa sifa ya kuwa kiongozi.

Hata hivyo uongozi wa klabu hiyo bado umeshindwa kufanya lolote la kumuadhibu Aggrey Morris, jambo ambalo kwa hakika linaleta mgawanyiko kwenye timu na kuweza kuiharibia Azam FC mipango yake hai ya kutaka kubeba ubingwa wa msimu huu pia kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa ambayo mwaka huu ndio itakuwa mara ya kwanza kwa klabu hiyo kucheza michuano hiyo tangu ilipopanda daraja takribani misimu minne iliyopita.

Kwa maoni yangu ikiwa Azam wantaka timu iwe na umoja na kuweza kuwa na mafanikio ya uwanjani lazima washughulikie suala hili katika namna inayofaa. Kama Aggrey Morris amekiri kuchukua rushwa basi aadhibiwe kama wengine ili kuwatendea haki wote walioadhibiwa na kuleta uwiano ndani ya timu. Endapo watamuacha kama ilivyo sasa bila kumuadhibu wala kuchukua hatua yoyote dhidi yao basi kuna wasiwasi mkubwa sula hilo likaleta ufa ndani ya timu - pia inaweza ikajenga tabia hiyo kwa wachezaji wengine - kwani wote wanajua kama fulani aliachwa kwa kosa kama hili basi hata yeye akifanya ataachwa kutokana labda na nafasi yake ndani ya kikosi cha Azam FC. Nini matokeo ya hali kama hii?

Matokeo yake timu itafanya vibaya na kuendelea kuzama katika siasa za mpira wa Kulwa na Doto, mwishowe matatizo ya vitu kama hivi ndio yanapelekea soka letu nzima kuoza na Tanzania kuwa nyuma kwa maendeleo ya mchezo huu.

Nawasilisha.    

7 comments:

  1. Hivi Enzi zile Pamba inafanya vizuri sikuwahi kusikia wachezaji wake wanachukua mlungula.

    Napata shida kufahamu, Tuangalie kiwango cha timu kwamba ni kidogo ndio wakafungwa au wachezaji hawako "MOTIVATED ENOUGH" ndio maana wanakubali kuhujumu timu.

    Tuwaulize wazee wetu waliongoza Pamba wao waliwezaje kupambana na njama za Kulwa na Doto?

    SIO PAMBA PEKEEE, Ushirika Moshi ikipiga soka safi, ilikuwa ni vigumu timu kama ya Kulwa au Doto kuishinda kwa kuizidi umilikaji wa Mpira. Wao walifanyaje?

    Au labda kiwango chao (Lamba lamba) kimeshuka tu ndio maana walizidiwa na mianya ya rushwa ikaingia au hao Kulwa na Doto ndio wanaopeleka umbea ili timu isambaratike wabaki peke yao.

    AZAM wasipokuwa makini hawaendi mbele.

    angalia utakapomkosa Agrey moris (Beki bora hata hao Kulwa na Doto zingependa kuwa nae) unapangiwa na timu kama TP mazembe, utafika popote kweli.

    Uongozi wa AZAM iangalie kwa kufanya (SWOT) upembuzi kwa nini wachezaji ambao wanalipwa vizuri na wapo motivated vizuri waihujumu timu?

    hivi Mbwana samatta anaweza kuihujumu TP Mazembe, fikiria Tresor (King) Mputu ahujumu timu ya TP kweli? Waende Study TOUR Lubumbashi wakaongee na Muisrael mwenye asili ya kikongo amewezaje?

    Azamu wanapesa na hawana pressure ya mashabiki kama kulwa na Doto, kwa hiyo wanaweza kupanga mipango taratibu na kumfukuza mwizi kimya kimya mwishowe wakafika na kumkamata kiuraini, lakini kwa kuwa wameaanza kujitengenezea pressure wenyewe basi wanaweza wasitimize malengo yao na hiyo sikufichi, NDIO NIA YA KULWA NA DOTO KUBAKI PEKE YAO BILA MPINZANI.

    WAENDE STUDY TOUR KWENYE VILABU KAMA TP MAZEMBE NA BONDENI WAJIFUNZE WAJE WASONGE MBELE. LAKINI WAKIKURUPUKA KAMA KULWA NA DOTO BAAAAAAAASI TUNARUDI KULE KULE.

    GEBO.

    ReplyDelete
  2. duh rushwa hadi kwenye soka jaman hii sasa kali na haileti maendeleo ya soka zaidi ya kurudi nyuma kwa timu kama azam ambayo wachezaj wake wanapata huduma zote bdo wanachukua rushwa wafungwe na yanga au simba kiukwel tanzania hatuwez kuendelea tutabakia simba na yanga zetu lakn maendeleo hayawez kuja hata siku kwa mtindo tunaokwenda nao.tafakar ndg mpenda michezo.

    ReplyDelete
  3. KULWA NA DOTTO NDIO WANAOHARIBU SOKA.IKITHIBITIKA WALITOA RUSHWA WASHUSHWE DARAJA.TFF MUPO?

    ReplyDelete
  4. Kaka naomba urekebishe article yako...Wote tumesikia taarifa rasmi ya Klabu ya Azam kuwa wachezaji hao walichukua RUSHWA kwenye mechi yao dhidi ya SIMBA SC (Dotto). Inakuwaje unamwingiza YANGA (Kulwa) kwenye sakata hili. Hivi mnataka kuonesha ushindi wa Yanga pia ulikuwa wa kimagumashi??? Tafadhali, msijitahidi ku-balance hata kwa equation ambazo hazi-balanci-ki.

    Ukweli ni kuwa Azam washikilie bango. Simba wamezoea kuhonga kwa Kado(kupitia kwa Ulimboka Mwakingwe), kwa Othumani Kazi kwenye mechi ya Majimaji ya Songea na lile tukio lisiloweza kusahaulika na wanamichezo makini la kiongozi wa Simba wakati huo Jabir Shikamkono kwa Kagera Stars ambapo mabao ya Fulgence Novatus na Nkama Ntare yalilifuta bao la penalti la Hussein Masha na hatimaye wachezaji wa Simba kulala mahabusu baada ya vurugu. Simba wajirekebishe ila viongozi wao waadabishwe na FIFA iwape "ban" ya maisha kwenye soka.

    ReplyDelete
  5. I am so shocked! sio kama mambo haya ni mageni katika soka letu, ila kutokea katika klabu kama Azam ambayo inawapa wachezaji wake kila kitu, lazima ujiulize mara mbili.

    Ikiwa Azam hivi, je? klabu kama Toto, prison, mtibwa na nyenginezo inakuwaje? hii ni issue kubwa haipaswi kuchukuliwa juu juu. I think its a good point to start. Ikiwa Azam wana strong evidence against those victims, TFF wanapaswa kuanzia hapa, badala ya kuendelea kuhubiri ugumu wa kupambana na rushwa katika soka letu. Inaonekana hata mentality ya wachezaji wetu ipo kirushwarushwa, How come? mchezaji anapata kila kitu halafu anakubali kupokea hongo ili aihujumu timu yake? nasema tuanzie hapa ili kulinusuru soka letu lisizidi kuelekea kuzimu.

    Bonta Zyuma

    ReplyDelete
  6. daaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah achana na hilo shaffih nina ushahidi wa kutosha boban kupewa mpunga na viongozi wa yanga apeleke moro simba ilipokuwa ikicheza game na polisi na mtibwa ili jamaa waharibu,jiulize boban kasimamishwa simba moro kaenda fanya nini?huu ufisadi kwenye soka sijui utaisha lini asee inakera sana tatizo tumewakabidhi wafayabiashara na wacheza kamali timu zetu ndo man wanatufanya hivi kwa maslahi yao ila wacha nikwambie akipatikana mtu wa kuwekeza pale ruvu shooting wale jamaa ni balaa hata azam,kulwa na doto hawagusi ule moto kama sio ubabaishaji wao wa kuhonga wanaumia bila kificho mi nimetazama game zao kadhaa wale jamaa hawana hela tu ila kiukweli wako vizuri sana shaffih.kin kibaden mputa aliyasema haya ya mlungula lakini tatizo tff hakuna watu pale amini nakwambia kuna mizigo ambayo haitakii mema mpira wetu,siwezi kuficha hisia zangu za chuki kwa bwana NGETA nilitegemea alichokua akikiandika atakuja kusahihisha kumbe daaaaaaaah kapata pa kulia asee kweli penye uzia penyeza rupia ndo alichokifanya bwana TENGA na yule bwana kayuni mganga wake inaonekana mpya sana mjini na hana foleni,mkurugenzi gani wa ufundi timu kila kukicha inashuka viwango vya fifa then jitu bado lipo tu ingekuwa amri yangu ningefungia huyu mtu asijihusishe na soka milele

    ReplyDelete
  7. Kwa azam sasa imekua jambo la kawaida kusikia hayo masuala ya rushwa.kosa kubwa walilofanya azam ni kuwachukua na kuwatumia watu wanaojiita watu wa mpira ili tu kuweza kua kama simba na yanga.sasa tujiulize watu hao ndio walioweza kufanya kuzifanya timu za simba na anga kua hapo zilipo wataweza vipi kuibadili azam?walicho fanya msim wa ligi iliyopita wakapata nafasi ya pili kila siku watu walikua wanasema kuhusu tabia za rushwa zilizokua zinaendelea.tulishudia kila timu iliokua ikacheza na azam ni matatizo tu.lkn baba wa soka TFF ikakaa kimya kana kwamba hakuna kinachoendelea.Azam ikaifunga yanga mara tatu mfululizo mara ya mwisho kila mtu anakumbuka kilichotokea kwenya soka letu Refa kapigwa kisa rushwa.bakhresa kama ana nia thabit na soka awaondoe watu hao wanaojiita wa mpira.arudi kwenya mipango yake alioanza nayo mwanzo.Tunaendelea kushuhudia kila inapofungwa na yanga kunatokea matatizo.VLADIMIR NIYONKURU,MRISHO NGASSA,STEWALT HALL,Sasa ERASTO NYONI,SAID MOURAD,AGGREY MORIS Hawa ni baadhi ya wahanga baada ya kufungwa na yanga.

    ReplyDelete