Search This Blog

Friday, November 9, 2012

SANTI CAZORLA, JUAN MATA NA MICHU WANUNUA HISA ZA UMILIKI WA TIMU NCHINI HISPANIA

Tumekuwa tukisikia namna wanamichezo wanavyotumia vibaya utajiri wao wanaopata katika fani zao, hasa wanasoka - huku wakiacha majukumu yao ya kurudisha kwa jamii katika kusaidia soka lizidi kupiga mbele zaidi, lakini jambo ambalo nimelisikia sasa limenifurahisha kiasi kujua kwamba kundi la wachezaji wa zamani wa Real Oviedo wamejiunga pamoja kuisadia timu yao inayokabiliwa na ukata mkubwa.

Santi Cazorla, Juan Mata na Michu wote ni wachezaji wa zamani wa Oviedo wakiwa wamekulia na kujifunza soka katika klabu hiyo na tunaambiwa kwamba watatu hao wamenunua hisa katika klabu hiyo ili kuikoa klabu hiyo kukaa vizuri kibiashara. 

Klabu hiyo ya Hispania, ambao kwa sasa wapo katika nafasi ya tano katika daraja la tatu la soka la Spain, ndio klabu ambayo Mata, Michu, na Cazorla wote walianzia maisha yao ya soka la kisasa katika klabu hiyo, Michu kwa kipekee zaidi alitumia muda mrefu zaidi katika klabu hiyo kabla ya kwenda Celta Vigo B.

Mie, Mata na Cazorla wote tumenunua hisa, lakini haitakuwa sawa kwangu mimi kusema ni hisa kiasi gani. Tumejaribu kuisadia klabu yetu ambayo wote tumeichezea," alithibitisha Michu.

Uchumi wa Hispania upo katika hali mbaya sana na klabu inahitaji kiasi kinachokaribia €2m ili kuweza kuendelea. Watu wengi wamenunua hisa  na tumaini letu sasa hali ya uchumi itaimarika kiasi mpaka kufikia mwisho wa ununuzi wa hisa tarehe 17 mwezi huu. 
"Hii ni klabu yangu ya nyumbani, klabu niipendayo, hivyo naamini mchang wetu na watu wengine utatosha kuisadia."

No comments:

Post a Comment