Search This Blog

Wednesday, November 7, 2012

CRISTIANO RONALDO: LIONEL MESSI SIO RAFIKI YANGU - NA HATUNA MATATIZO YOYOTE

Cristiano Ronaldo amesema ana mahusiano ya kazi tu na mpinzani wake Lionel Messi  na sio marafiki na nyota huyo wa Argentina na Barcelona

Wawili hao wamekuwa wakishindanishwa kwa kila kitu  katika miaka ya hivi karibuni, huku wachezaji wote wawili wakicheza kwa jitihada kubwa kushinda makombe na tuzo binafsi. Hta hivyo japo anakiri kwamba hakuna urafiki wa karibu, Ronaldo anasisitiza hawana ugomvi na Lione Messi na pia akazungumzia heshima yake kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona. 

"Yeye [Lionel Messi]ni mchezaji mzuri na mkubwa sana ," Ronaldo aliiambia beIN sport. "Nina mahusiano ya kikazi tu na yeye kama niliyonayo na wachezaji wengine. Messi sio rafiki yangu. kwa sababu hatushei chumba cha kubadilishia nguo. Namheshimu kama mchezaji. Sisi sio marafiki, japokuwa tuna mahusiano ya kikazi tu.

"Hakuna ugomvi wowote kati yetu japokuwa kuna baadhi ya watu wanajaribu kutengeneza hali ya namna hiyo, na sio kitu kipya kimekuwa kikitokea kwa takribani miaka mitano iliyopita. Siwezi kukizuia."

Ronaldo aliendelea mbele na kusema kwamba anaweza kucheza na Messi timu moja, kitu ambacho hata hivyo amekiri ni kigumu.
"INaweza nikacheza vizuri sana na yeye ikiwa tu atasaini kujiunga na Real Madrid, lakini hilo ni gumu sana," anasema Ronaldo.

No comments:

Post a Comment