Cesc Fabregas na girlfriend
Daniella Semaan wamekuwa kwenye mapenzi mazito katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita. Walionekana wakila raha hivi karibuni wakati wa kipindi cha kiangazi huko Italy - lakini sasa kidudu mtu kimeanza kuingia kwenye mapenzi yao.Aliyekuwa mume wa mchumba wake Fabregas, Millionea Elie Taktouk amejitokeza na kusema kwamba ulikuwa ndio wakati huo wa mapumziko ya kiangazi alipogundua mkewe anamsaliti - wakati wakiwa wanajaribu kupata mtoto wa tatu.
Millionea huyo amekuwa akizungumzia maumivu aliyoyapata juu ya usaliti wa mkewe aliyekuwa akiufanya na mchezaji wa Barcelona mwenye miaka 25.
Danielle Semaan, 38, na Elie wameshatalikiana, kama ambavyo anasema kwamba baada ya kuona picha za mkewe na Cesc, akaona ni bora aachane na mkewe huyo.
Wanandoa hao wawili wana watoto wawili, mtoto wa kiume mwenye miaka 11 na wa kike mwenye miaka 8.
Eli Taktouk(kushoto), akiwa na rafiki yake.

No comments:
Post a Comment