Search This Blog

Wednesday, November 7, 2012

DADA WA MSHAMBULIAJI WA KIBRAZIL HULK ATEKWA NYARA

Dada wa mchezaji wa  Zenit St Petersburg  Hulk ametekwa nya nchini Brazil, maofisa wa kituo cha polisi cha eneo la Campina Grande wamethibitisha.

Angelica Aparecida Vieira alikuwa nje ya mgahawa ambapo anafanya kazi siku ya Jumatatu katika eneo la Brazilian City.

Msichana huyo mwenye miaka 22 alichukuliwa kutoka kwenye gari lake mwenyewe na kuwekwa kwenye gari la watekaji kwa mujibu wa meneja wa mgahawa Helio da Silva ambaye alishuhudia tukio hilo, na alipata mshtuko wa moyo na ikabidi apelekwe hosptali lakini sasa ameachiwa.

Polisi bado hawajathibisha ni watu wangapi walihusika na utekaji nyara huo, ambao ulitokea muda wa 8 mchana kwa muda wa Brazili.

Hulk hakuwa amepangwa kucheza mechi yao ya leo usiku ya Champions League dhidi ya Anderletch kutokana na majeruhi ambayo yatamuweka nje ya dimba kwa wiki mbili.

No comments:

Post a Comment