Search This Blog

Thursday, September 27, 2012

UAMUZI WA NEYMAR KWENDA ULAYA - MKUBWA ZAIDI TANGU MESSI ALIPOSAINI BARCELONA KWA KUTUMIA LESO


Lionel Messi alikuwa na miaka 13 tu alipojiunga na Barcelona. Hakukuwa na vita yoyote ya kugombea saini yake, na mkataba wake ulisainiwa kwenye leso haukuwa na shamra shamra nyingi wala kuwasili kwake Nou Camp. 


Messi hakuchagua sehemu bora kwake; alikuw na chaguo moja na ndilo alilochagua. Barcelona ndio ilikuwa klabu pekee iliyokuwa tayari kulipa fedha za kumtibu ugonjwa wake wa upungufu wa homoni, na kutokana na imani yao kwa kijana huyu wa Kiargentina leo hii dunia inashuhudia ladha ya soka na klabu inanufaika.

 "Nilihitaji fedha kwa ajili ya dawa zangu kunisaidia niweze kukua na Barcelona ilikuwa ndio klabu pekee iliyotoa ofa. Hivyo mara tu walipokubali kunitibia nikajua nitakiwa kuondoka nyumbani na kwenda Catalan," Messi aliliambia jarida la Match of the day. Hiyo ilikuwa mwaka 2000. 

Miaka 12 tangu wakati huo kutoka sasa, Messi ameibuka kuwa mchezaji bora kabisa katika kizazi hiki - akiiongoza Barcelona kupata mafanikio makubwa kuliko katika historia ya klabu hiyo, kuanzia nyumbani mpaka ulaya, huku akitajwa mara 3 kuwa mchezaji bora wa dunia (2009,2010, 2011).

Barcelona ingekuwaje bila kuwepo kwa Messi? Unapoangalia takwimu zake za mabao, na mchango wake wote kwa ujumla na namba ya mechi alizocheza kwa kiwango kikubwa na kuipa ushindi Barca, kuna hitimisho moja tu: Wasingekuwa na mafanikio haya au wangekuwa duni kama ilivyokuwa miaka ya 90.

Je wangekuwa wameshinda makombe matano ya La Liga, mawili ya Spanish Super Cup na matatu ya ulaya ambao wameshinda wakati wa uwepo wa Messi?

Ofcourse wasingeweza. Hivyo sio kusema timu za Frank Rijkaard na Pep Guardiola zingetoka mikono mitupu, kwa sababu bila Messi pia walikuwa na timu nzuri kulinganisha na vikosi vya timu nyinginezo barani ulaya. Lakini ni mara ngapi   tumeishuhudia Barca ikicheza vizuri bila uwepo wa Messi au akiwa yupo chini ya kiwango?

Ukiangalia nyuma, unaweza kusema uamuzi wa Messi kuondoka nyumbani kwao Argentina na kujiunga Barcelona ndio ulikuwa uamuzi uliobadilisha hatma ya soka la ulaya ndani ya miaka 10 iliyopita.

Ni wazo ambalo linatuleta kwa Neymar - mtu ambaye wengi wanamtaja kuwa Messi mpya ambaye ana machaguo mengi katika timu kubwa za ulaya tofauti na ilivyokuwa kwa Lionel.

Hali ya Neymar ni tofauti sana na ilivyokuwa kwa Messi mwaka 2000. Kijana huyu wa Kibrazil tayari ni jina kubwa sana kwenye soka na tayari ameshaanza kuitawala soka ya dunia.

Ni shujaa wa kuteuliwa pale Santos - akifuata nyayo za Pele - huku akitajwa kuwa ndio mchezaji anayetazamwa kuwa bora zaidi katika miaka 10 ijayo katika ulimwengu wa soka.

Uhamisho kwenda Ulaya ni jambo ambalo linangoja muda tu, kitu ambacho kinaeleza kwanini Neymar amekuwa ndio mchezaji anayeandikwa sana kwenye tetesi za vyombo vya habari katika kipindi cha miaka 3. Kila mtu anajua anaondoka Brazil, lakini ni wachache sana au kuna hakuna anayejua kwa hakika ni lini, ni wapi na jezi ya timu gani atakuwa akivaa huko Ulaya.

Mbrazili mwenzie Dani Alves ni mmoja ya wengi wenye matumaini ataungana na Messi pale Barcelona - dili ambalo mwandishi wa ESPNsoccernet, anaamini limeshafanyika.

Ni kitu cha kusisimua sana kumuona Neymar akiungana Messi, lakini pia kama ilivyo kumuona akiungana na Cristiano Ronaldo pale Real Madrid, Eden Hazard pale darajani Chelsea, Wayne Rooney na Robin van Persie pale Old Trafford au kuungana na David Silva na Sergio Aguero pale Etihad Stadium na Man City.

Timu zote kubwa barani ulaya kwa sasa zimetajwa kuwa zinaweza kumchukua mchezaji huyo, huku gazeti la Metro likiripoti kwamba klabu ya PSG ipo tayari kulipa £85 million mwezi January kumsaini kinda huyo.

Pia kumekuwepo na mawazo kwamba Santos hawatomuuza mchezaji huyo mpaka litakapofanyika kombe la dunia 2014,  lakini bei ya Neymar sokoni inapanda, ni vigumu kuamini kwamba wataweza kuimiri na kukataa fedha nyingi katika kipindi cha madirisha matatu makubwa ya usajili yajayo.

Uamuzi wa Neymar kuondoka Brazil - utamaanisha kumpa nafasi kubwa ya mchezaji bora wa kizazi chake kwenye soka. kwa kipaji alichonacho, ana kila kitu cha kumfanya aweze kuitawala soka ya ulaya na kuipeleka timu atakayoichagua katika levo nyingine ya mafanikio - sio tu uwanjani bali pia katika biashara na kuifanya kuwa kubwa zaidi ya ilivyo sasa.

1 comment: