Michuano
ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi
ya pili kesho (Septemba 19, 2012) kwa timu zote 14 kuumana
katika viwanja saba tofauti nchini.
Wakati
Simba ikiwa mgeni wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa Yanga kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini
Morogoro.
Viingilio
kwa mechi ya Uwanja wa Taifa vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000
na sh. 20,000 wakati kwenye Uwanja wa Jamhuri itakuwa sh. 3,000 kwa sh.
10,000.
Mechi
nyingine za ligi hiyo zitakazochezwa kesho ni African Lyon vs Polisi
Morogoro kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Nayo Ruvu
Shooting itashuka kwenye Uwanja wake wa Mabatini, Mlandizi kuikabili
Mgambo Shooting kutoka Handeni mkoani Tanga.
No comments:
Post a Comment