Search This Blog

Tuesday, September 18, 2012

UTANI WA MANCINI KWA MOURINHO: MRUDISHE RONALDO KWAO KWA MIEZI 6 KAMA MIMI NILIVYOMFANYIA TEVEZ



Manchester City  na Real Madrid wanaanza kampeni yao ya Champions league katika kundi la kifo kwa kukutana wenyewe. Kuelekea kwenye mechi, wote wawili Jose Mourinho na Roberto Mancini wamekuwa wakitupiana vijembe vya hapa na pale kupitia media na katika mkutano wa waandishi wa habari wa Mancini, alitoa ushauri kwa Real Madrid manager namna ya kushughulikia suala la Cristiano Ronaldo.

Kifupi, Mancini amesema kwamba itabidi Mourinho amrudishe Ronaldo kwao kwa miezi sita ya msimu kama ambavyo yeye alivyomtimua Carlos Tevez kutoka katika kikosi cha City mwaka jana kabla ya kumrudisha na kumsaidia kushinda ubingwa wa ligi kuu ya England.

Mancini alitania:
 
   "Ikiwa Mourinho anataka kushinda tena La Liga nafikiri inabidi amuondoe kikosini Cristiano kwa miezi 6 na ampeleke Ureno, na baada ya hapo amrudishe, wanaweza kushinda La Liga kwa mara pili. (Akicheka) Sijui lakini nadhani itakuwa ni hali tofauti. Lakini hii ilifanya kazi kwetu mwaka jana - na kwa hili sitanii ni kweli Carlos Tevez aliporudi mwezi January alitusaidia na tukaweza kushinda ubingwa wetu wa kwanza katika kipindi cha miaka 50."

No comments:

Post a Comment