KILA
ifikapo mwishoni mwa msimu wa ligi kuu kila nchi kupitia ligi huwa na
utaratibu wa kutoa tuzo mbalimbali kwa wachezaji waliofanya vizuri
kupitia nyanja mbalimbali.
Katika
soka utaratibu huo upo ambapo timu inayoibuka na ubingwa hupata kombe
huku mchezaji bora, mwanasoka mwenye nidhamu, mfungaji bora, golikipa
bora nao wakipata tuzo zao.
Katika ligi kuu ya soka nchini Hispania maarufu kama Primela La Liga zipo tuzo kadhaa ambazo hutolewa ikiwemo ya mfungaji bora.
Tuzo hii ya mfungaji bora hutolewa kila msimu kama ilivyo kawaida na imepewa jina la Pichichi Trophy.
MIONGONI MWA WASHINDI WA PICHICHI
Mchezaji
Diego Forlan amewahi kushinda mara mbili tuzo ya Pichichi (tuzo ya
mfungaji bora katika Ligi Kuu ya Hispania), ambapo mara ya kwanza
alishinda msimu wa 2004-05 wakati alipokuwa kwenye timu ya Villarreal na
mara ya pili msimu wa 2008-09 akiwa klabu ya Atletico Madrid.
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi alitwaa pichichi katika msimu wa 2009-2010,2011-2012.
Naye Cristiano Ronaldo alitwaa pichichi katika msimu wa 2010-2011.
Msimu wa 2007-208 mwanasoka Danny Guiza wa klabu ya Mallorca alitwaa pia kiatu cha dhahabu katika msimu wa ligi ya Hispania.
KWANINI TUZO HUITWA PICHICHI?
Kwanini tuzo ya mfungaji bora wa ligi kuu ya Hispania huitwa jina la Pichichi?
Ukweli
ni kwamba asili ya neno pichichi katika tuzo ya mfungaji bora nchini
Hispania imetokana na aliyekuwa mwanasoka wa klabu ya Athletic bilbao
Rafael Moreno Aranzadi maarufu kama Pichichi ambaye alifunga mabao mengi
wakati akiichezea Bilbao katika miaka ya 1910 hadi 1920.
Katika miaka hiyo Rafael Moreno ‘Pichichi’ aliifungia Bilbao jumla ya mabao 200.
Pichichi
ambaye alizaliwa mwaka 1892 alifariki dunia mwaka 1922 na mara baada ya
kifo chake, gazeti maarufu la michezo nchini Hispania la Marca
likaandaa tuzo ya mfungaji bora na kuipa jina la Pichichi kama njia ya
kumuenzi mwanasoka huyo.
NINI MAANA YA NENO PICHICHI?
Pichichi
ni neno la Kihispaniola ambalo ukilitafsiri kwa kiingereza unapata neno
Little Duck ambalo kwa Kiswahili Little Duck tunasema Bata Mdogo.
BRAZIL WANGEIITAJE?
Katika
miaka ya zamani gwiji Pele ndilo lilikuwa linatamba huko nchini Brazil
hasa kwa umahiri wa kupachika mabao mengi zaidi ikiwemo kwenye klabu na
hata timu ya taifa.
Pengine tuzo ya mfungaji bora katika nchi ya Brazil wangeiita Pele Trophy kama sehemu ya kumpa heshima gwiji huyo.
TUZO YA GOLIKIPA BORA(ZAMORA TROPHY)
Tuzo
hii pia bado inaendelea kutolewa huko Hispania kwa upande wa
mlindamlango bora ambaye amefanya vizuri katika msimu mzima wa ligi kuu
ya Hispania.
Tuzo hii pia hutolewa na gazeti la Marca ambapo kwa mara ya kwana ilikuw amwaka 1958.
Jina
la Zamora limejitokeza kwenye tuzo hii kutokana na heshima ya kumuenzi
mkongwe huyo aliyezaliwa mwaka 1901 na kufariki mwaka 1978.
Katika
enzi zake Zamora aliweza kuokoa michomo mingi na kuwa golikipa hodari
wakati akizichezea timu za Espanyol, Barcelona,Real Madrid na Nice kati
ya mwaka 1916 na 1938.
MASHARTI YA TUZO YA ZAMOURA
Golikipa
anapaswa awe amecheza mechi zisizopungua 28 katika msimu na katika
mechi hizo kila moja awe amecheza kwa muda usiopungua dakika 60.
Sharti
la pili ni kwamba haijalishi magolikipa wangapi wamefanya vizuri ndani
ya msimu mmoja kw amaana kwamba kila golikipa atakayefanya vizuri
atapata tuzo ya Zamora hata kama rekodi zao zikifungana.
La
tatu ni kwamba golikipa anatakiwa awe ameruhusu idadi ndogo sana ya
mabao ya kufungwa. Hapa huchukuliwa idadi ya mabao aliyofungwa na kisha
hugawanya kwa idadi ya mechi alizocheza ambapo majibu yake ya wastani
huja katika mfumo wa desimali.
Makala haya yameandaliwa na Arone Mpanduka(Radio Tumaini) kwa msaada wa mtandao wa Intaneti.Barua Pepe mpanduka@yahoo.com.0713 896320
No comments:
Post a Comment