Search This Blog

Friday, July 13, 2012

MILOVAN WA SIMBA: ASEMA HARIDHISHWI NA VIWANGO VYA BOBAN, KAZIMOTO NA NYOSSO

KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic amesema kuwa kikosi chake hakipo imara katika kiwango kile anachokihitaji kwa ajili ya Michuano ya Kagame.

Hayo aliyasema muda mchache baada ya mechi ya fainali kati ya timu yake na Azam FC, mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2 na badaye kupiga penati na Simba kushinda mabao 3-1, mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa.

Milovan alisema, Kagame ni michuano mikubwa yenye upinzani mkubwa kutokana na kila timu kujiandaa kwa kuchukua ubingwa.

Kocha huyo aliwataja wachezaji ambao viwango vyao havijamridhisha bado Haruna Moshi ‘Bobani’, Mwinyi Kazimoto, Juma Nyosso na Amir Maftar .

Alitaja sababu ya kutokuwa fiti ni mapumziko ya wiki mbili yamesababisha wachezaji hao kuwa imara katika viwango vyao vilivyozoeleka uwanjani, hivyo amepanga kuwapa mazoezi ili kurejesha hali yao ya mwanzo.

Simba inatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza Jumatatu ijayo dhidi ya URA ya Uganda saa 10:00 jioni na mchezo mwingine utapigwa kati ya Villa Club na Ports saa 8:00 mchana Uwanja wa Taifa.
mwisho 

No comments:

Post a Comment