Search This Blog

Friday, July 13, 2012

KOCHA WA YANGA: NINA KIKOSI BORA CHA KUTETEA UBINGWA WA KAGAME


WAKATI akijiandaa kuvaana na wapinzani wake Atletico ya Burundi, Kocha Mkuu wa Yanga, Tom Saintfiet ametamba kuwa kikosi kipo fiti.

Yanga ambao Mabingwa wa watetezi wa Kombe la Kagame wanatarajiwa kucheza na Atletico kesho jioni saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kocha huyo ambaye raia wa Ubeligiji amesema maandalizi ya siku chache tangu afike akae pamoja na kikosi zinatosha kutetea taji hilo la ubingwa.

Mbeligiji huyo amesema, atajitupa uwanjani kesho huku akiwa na hofu kubwa dhidi ya wapinzani wake kutokana na ukubwa wa michuano hiyo .

Katika hatua nyingine, Kocha huyo amesikitika kuwakosa wachezaji makinda, Frank Domayo, Simon Msuva na Omega waliopo kwenye kambi ya Timu ya taifa ya vijana ya U-20 inajiandaa kucheza na Nigeria katika mashindano ya vijana ya Afrika ya umri wao .

Yanga ipo kundi C na timu ya APR, Wau Salaam watakaocheza nao kesho, mechi itakayoanza kuchezwa majira ya saa ya 8:00 mchana Uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment