Search This Blog

Friday, July 13, 2012

KALI YA LEO: MARADONA AKATAA KUTAMBUA UAMUZI WA AL WASL KUMFUKUZA

Makocha wengi wanapokuwa wamefukuzwa, wanapaki mabegi yao, wanaaga wachezaji wao na benchi la ufundi, na kutoa taarifa kwa media kuelezea namna ambavyo maisha yao yalivyokuwa ndani ya klabu na kistaarabu watawatakia mema mabosi wao katika kuiendeleza klabu. Diego Maradona hayupo hivyo, siku moja baada ya kufukuzwa na klabu ya Al Wasl, muargentina huyo ametangaza kwamba bado anataka kuendelea kuifundisha klabu hiyo.

"Napenda kusema kwamba siku imekuwa ni nia yangu kuendelea kubaki kwenye nchi hii nzuri ambayo siku zote imekuwa ikinipokea vizuri, ninawashukuru sana kwa hili hasa Sheik kwa kunipokea na kunipa nafasi ya kufundisha klabu ya Emirate," taarifa iliyotolewa na Maradona inasomeka.

"Ukweli ni kwamba katika siku za mwisho, tumekuwa tukiongea kujaribu kukubaliana kuhusu ununuzi wa wachezaji wapya, ni hitaji ambalo nililihitaji kwa ajili kuweza kutimiza mipango yangu ya kushinda ligi kwa matokeo mazuri.

"Siku zote nitakuwa mwingi wa shukrani kwa mwajiri wangu na ningependa kuweka hili wazi kwamba nilikuwa na furaha siku zote nikiwa klabuni na jinsi walivyonipa sapoti. Lakini kwa bahati mbaya, klabu imetoa taarifa ambayo siisapoti kwa sababu bado nataka kuendelea kuifundisha Al Wasl.

"Kama haiwezekani klabu kununua wachezaji wapya kwa sababu hawana fedha za kufanya hivyo, basi kuna uwezekano mkubwa tukakaa na kulijadili hili pamoja na bodi kujaribu kupata suluhisho. Natumaini kutakuwa na kikao chetu hivi karibuni tujadili hili suala. Nina uhakika wapo tayari kujadili hili na tutafikia makubaliano mazuri tu."

No comments:

Post a Comment