Search This Blog

Friday, June 8, 2012

TETESI HAI: YANGA YAFANYA BALAA LINGINE SIMBA - OKWI KUTUA BONGO KUMALIZANA NAO.

Sekeseke la usajili limeendelea kupamba moto.

Katika kuhakikisha wanaibomoa kabisa safu ya ushambuliaji wa watani wao iliyowafunga kipigo cha aibu cha mabao 5-0 katika mechi ya kufunga msimu uliopita. Klabu ya bingwa ya afrika mashariki na kati, Dar Young Africans inakaribia kumnasa mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda na tegemeo la klabu ya Simba, Emmanuel Okwi.

Taarifa za udaku nilizozipata kutoka ndani ya Yanga ni kwamba timu yao ipo tayari kulipa fedha wanazozitaka Simba ili kuweza kupata huduma za Okwi msimu ujao. Taarifa zinasema kwamba Okwi ambaye kwa sasa yupo nchini Uganda anatarajiwa kutua Tanzania ndani ya kipindi cha masaa 72 kuja kumaliza suala la usajili wake kwenda Yanga ambao inasemekana wamemuhaidi fedha nyngi sana.

10 comments:

  1. Kama ni kweli hii na ikatokea Yanga wakafungwa tena basi itabidi wajiangalie upya, tuliona haya wakati wanamsajili Haruna Niyonzima, walichonga hivi hivi matokeo yake ngao ya hisani wakachezea kichapo, mechi ya ufunguzi dhidi ya JKT ruvu wakachezea kichapo, na hatimaye wakakosa hata nafasi ya pili, kama ni kweli Okwi na Yanga tunawatakia kila la heri isije kuwa turufu za uchaguzi na kupooza kipigi cha tano bila.

    ReplyDelete
  2. Mpira wa Tanzania unashabikiwa na wajinga wengi na ndio maana hauwezi kuendelea sasa washabiki wa Yanga wanaona maendeleo sana ndio hayo wkt ukuta pale uwanja wa kaunda umedondoka mwaka wa 3 huu wanachotwa akili ili wamuuzie timu Manji kijanja kwa kumpa uenyekiti kama anahela si aanzishe timu yake kama Bakhresa na Azam FC why aingilie Yanga.

    ReplyDelete
  3. tusha waambia nyinyi simba masikini uwezo wa kuchukua first eleven yenu yote tunao,tutamaliza wote nyie endeleeni kumruhusu huyo rage kufungua bakuli lake tuta vuruga timu nzima.kaeni kimya wanaume tupo kazini

    ReplyDelete
  4. kwi kwi kwi okwi ni simba na simba ni okwi, bila okwi hakuna simba yaani jamaa akisepa tu simba kwisha habri yake, aden rage atafute pa kwenda maana gogoro litakaloibuka hapo mungu hapendi

    ReplyDelete
  5. okwiiiiiiiiiiiiiii yupo austria kujaribu soka la kulipwa, hwezi kuhangaika na wazee wa SUPA 5.

    ReplyDelete
  6. Simba sio okwi kaka,anaweza kuondoka na simba ikasimama kama kawa,simba wana uwezo wa kupata sriker mwingine wa hadhi yake,mafanikio ya Yanga hayaji kwa kuibomoa simba ila wajipange vizuri,yote hiyo ni kiwewe cha kipigo cha 5-0

    ReplyDelete
  7. Nafikiri YANGA WAJIULIZE KWA NINI MDA WOTE WANACHUKUA MCHEZAJI MSIMBA,,? SIMBA WANASAJILI WACHEZAJI WALIO NA UWEZO UWANJANI HILO HILO HALINA UBISHI LAKINI YANGA NYIE MNASAJILI KWA SIFA TU KWASABABU MNA UWEZO KIFEDHA,, KUNA WATU PALE SIMBA WAPO KIMYA SANA NA NDIO HAO WANAFANYA KAZI YEYE RAGE ANAWAZUGA TU KWA KELELE ZAKE ILI MSIONE WACHEZAJI WAZURI MKALIE KUFIKIRIA KUMJIBU,, MWISHO WA USAJILI NDIO TUTAONA NANI AMESAJILI WACHEZAJI WENYE UWEZO UWANJANI, HONGERENI YANGA WAZEE WA MANJI,!

    ReplyDelete
  8. Huyo kuku anayesema simba ni okwi,huyo okwi alikuwepo tangu mwaka 1936 simba ilipoanzishwa,fikiria kwanza ndo uanze kubwabwaja.

    ReplyDelete
  9. aliondoka samatta sembuse okwi majembe bado mengi subirini ligi ianze mtamfukuza maximo muda mfupi tu. mnakubuka kombination ya patric ochan na samata sasa inatesa tp bado simba pia inatisha yupo messi atafanya mambo.hapo vipi

    ReplyDelete
  10. acheni mambo yenu nyie,hayo ndiyo maendeleo ya soka!dunia nzima sasa hiv wanajua mpira ni pesa kama hauna pesa kaa pembeni.swala la ukuta wa kaunda sio la manji hilio ni jukumu la tff na serikali yake,bakhresa ni bakhresa na manji ni manji hauwezi kumpangia mtu matumizi ya pesa zake!wachezaji nao wanahitaji maisha bora na hapo ndio sehemu yake! mpira ni pesaa...!!!!

    ReplyDelete