Search This Blog

Friday, June 1, 2012

STARS YAWASILI ABDIJAN, KIM ASEMA MECHI ITAKUWA NGUMU

Kikosi cha Taifa Stars kimewasili hapa Abidjan (Mei 31 mwaka huu) mchana huku Kocha Mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen akisema mechi dhidi ya Ivory Coast itakuwa ngumu. Stars yenye wachezaji 21 ilikuwa iwasili hapa asubuhi, lakini ndege iliyobadilisha Nairobi ilichelewa kuondoka kwa saa tatu.

 Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na wenyeji Ivory Coast (Tembo) itachezwa Juni 2 mwaka huu Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny kuanzia saa 11 kamili jioni ambapo Tanzania itakuwa saa 2 kamili usiku.

Licha ya kwanza, Stars ililazimika kuacha wachezaji wawili dakika za mwisho (Haruna Moshi na Nassoro Cholo), Kim amesema kikosi chake ambacho kimefikia hoteli ya Ibis bado kimejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo. “Tunaiheshimu Ivory Coast kwa vile ni timu ambayo inaundwa na baadhi ya wachezaji nyota wa dunia kama akina Drogba (Didier) na Yaya (Toure), lakini wajiandaa kupata wakati mgumu kutoka kwetu,” amesema Kim ambayo kikosi chake baada ya kuwasili hapa kilipata fursa ya kufanya mazoezi jioni.

1 comment:

  1. shafii jamaa wa skysport ni vp?mbona logo ya chama cha soka tanzania wametuwekea ya FAT? kwenye ratiba ya ya gemu ya kesho utawala wa kina ndolanga kumbe bado upo?he he saidia hawa jamaa

    ReplyDelete