Peter Schmeichel anarudi Manchester United.
Mchezaji huyo wa Red Devils anarudi Old Trafford ilimkuja kuwa balozi rasmi wa klabu hiyo kama ilivyo kwa wachezaji wengine kama Bryan Robson na Gary Neville - lakini bado haijawekwa wazi kama atahusika na benchi la ufundi au la.
Kumekuwepo na hisia za furaha ndani ya klabu hiyo juu ya habari za kurudi kwa mdenmark huyu ambaye aliichezea United kwa mafanikio makubwa.
Mchezo wake wa mwsiho kuichezea United ulikuwa mchezo wa fainali ya Champions league dhidi ya Bayern Munich pale Nou Camp, ambapo mdenmark huyu alipanda mbele dakika za mwisho huku timu yake ikiwa nyuma kwa bao 1 kwenda kushambulia kona iliyopigwa na David Beckham na kupelekea goli la kusawazisha la Teddy Sheringham katika muda wa nyongeza.
Welcome legend.
No comments:
Post a Comment