Search This Blog

Friday, June 22, 2012

KWANINI SIMBA NA YANGA ZIMEKUWA NA KASUMBA YA KUWA NA MALIMBIKIZO YA MADENI YA MISHAHARA?

Moja ya sababu kubwa zinazotufanya watanzania tusiendelee kwenye upande wa soka ni kukosa uongozi bora kuanzia kwenye vyama vya soka mpaka kwenye vilabu.


Siasa imewatala sana viongozi wa soka kiasi kwamba mpaka kwenye vitu ambavyo siasa hahitajiki tunajaribu kuiweka ili tuweze kufanikisha malengo yetu binafsi. Suala hili ni moja ya matatizo makubwa yanayoikumbuka soka letu la Tanzania, hasa kwenye vilabu vyetu vikubwa vya Simba na Yanga.


Navitaja vilabu hivi kwa sababu kiukweli lazima tuseme kwamba ndio nguzo kuu ya soka la Tanzania, vyenyewe vinapokuwa vinaboronga basi kwa kweli na soka letu linayumba. Vilabu hivi siku zote vimekuwa vikikosa viongozi wenye mawazo endelevu ya kuvifanya vilabu hivi kuendelea mbele. Moja ya matatizo makubwa yanayosababishwa na uongozi mbovu wa vilabu hivi ni mfumo wa usajili.


Usajili wa Simba na Yanga siku zote unafanywa kihuni, mtu yoyote ambaye anaweza kujiita mdau anaweza akamsajili fulani kwa kutumia fedha zake bila baraka za benchi la ufundi aidha kwa kutaka sifa au kujipigia kampeni kwa kutaka uongozi ndani ya klabu, na mwisho wa siku wachezaji wanaosajiliwa muda mwingine wanashindwa kuingia kwenye mipango ya kocha kwa kuwa labda hakuwa anawahitaji kwenye timu yake.


Pamoja na matatizo yote yanayovikabili vilabu hivi lakini leo katika makala yangu hii nitabase kwenye upande wa usajili. Nasukumwa kuandika makala hii kutokana na hali inayoendelea kwenye vilabu vyetu Simba SC na Dar Young Africans ambao kwa sasa hawana kocha baada ya kocha mkuu Mserbia Kostadin Papic kuondoka.


UPANDE WA YANGA


Yanga ambao kwa sasa wapo katika mchakato wa kufanya uchaguzi baada ya ule uongozi uliokuwepo chini mwanasheria Lloyd Nchunga kujiuzulu, hawana kocha mkuu, lakini cha ajabu timu hiyo inafanya usajili wa wachezaji ambao wanasajiliwa na watu wanaojiita wadau au wanachama wa klabu hiyo. Kesi ya suala la kiufundi tuiache pembeni kwa leo kwa usajili wa wachezaji tuangalie kwa upande wa kiuchumi.


Moja ya matatizo makubwa yaliyoukumba uongozi wa Lloyd Nchunga ni madeni pamoja na malimbikizo ya mishahara na fedha za usajili. Mmoja ya viongozi waliojizulu kwenye uongozi uliopita anasema: "Wakati tupo madarakani tulipatwa na matatizo mengi ya kifedha kwa mfano suala la mishahara. Wachezaji walisajiliwa na kikundi cha watu ambao ni wadau wa Yanga, wakaingia nao makubaliano kwa niaba ya Yanga kwa mfano utakuta wachezaji wamesaini mkataba wa miaka miwili kwa kulipwa mshahara wa dola 1000 mpaka  5000 kwa kiwango cha juu kwa mwezi na posho mbalimbali, wakati ukija kwenye bajeti halisi ya mwezi utakuta fedha yote tuliyonayo inazidi tunayotakiwa kulipa. Na hapo ndipo malimbikizo ya madeni ya mishahara yalipoanza kuzidi. Hili suala lilitokea kwa takribani wachezaji wote pamoja na hata kwa upande wa kocha.
'Pia kulikuwepo na madeni ya fedha za usajili, utakuta fulani anamsajili mchezaji kwa makubaliano ya millioni 30, labda anampa shilingi milioni 20 na 10 zilizobakia anahaidiwa kumaliziwa baadae, muda unapofika mchezaji anapohitaji kumalizia fedha zake, uongozi unashindwa kwa sababu fedha hizo zinakuwa hazipo kwenye bajeti."


Haya sasa hivi Yanga ikiwa haina kocha wala uongozi mkuu, timu imeshasajili wachezaji wasiopungua watano wapya kwa fedha ambazo zinatolewa na kikundi cha wadau wa Yanga, na kama ilivyo kawaida msaada wao wakishamaliza usajili wanauachia uongozi mahitaji mengine ambayo mwisho wa siku yanakuwa yanazidi bajeti nzima ya klabu kwa ajili ya kugharimia matumizi. Hivyo kupelekea timu kujawa madeni na wachezaji kuwa na migomo isiyoisha.
Mwisho wa siku hata huu uongozi mpya unaotarajiwa kuingia madarakani utakutana na hicho kimbembe kwa kuwa haukuhusika kwenye mchakato wa kuwasajili wachezaji.


Kwa hali hii timu itafanya vipi vizuri kwenye michuano inayoshiriki? Hivyo wito wangu kwa wanayanga kuangalia juu ya suala hili la usajili kwa umakini, kama halitowasumbua kiuchumi ikiwa wenye pesa wataingia madarakani basi litakuwa na madhara kiufundi kutokana na usajili kufanywa na watu wasiohusika na benchi la ufundi - nasema kwa kuwa timu sasa inatafuta kocha na bado inasajili mwisho wa siku ndio matatizo ya miaka yote yanaendelea kuikumba klabu hii.

KWA UPANDE WA SIMBA
Simba nao hawana tofauti na ndugu zao Yanga, ingawa wenyewe atleast kwa sasa bado wana kocha na uongozi ukiwa bado upo madarakani.
Lakini linapokuja suala la usajili ishu ipo vile vile kama kwa wenzao Yanga, viongozi ndio wanaosajili wachezaji na sio kocha, ikumbukwe takribani mwezi mmoja uliopita niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari "UONGOZI MBOVU: KABURU AMSAJILI ABDALLAH JUMA BILA KUPATA BARAKA ZA KAMATI YA UFUNDI".
Hili ni tatizo kubwa sana, yaani mambo yanakwenda ovyo ovyo ndani ya hizi timu mbili, kiongozi mkuu yeye ndio anafanya kila kitu, kulipa mishahara yeye, posho yeye, hata kusajili yeye. Sasa kocha na kamati yake ya ufundi wao kazi yao nini? Hilo moja.


La pili kwenye kusajili wachezaji hao hao, kama ilivyo kwa Yanga, Simba nao wamekuwa na mfumo wa kikundi cha wadau wenye fedha kumsajili mchezaji wanayemtaka na kumleta kwenye timu huku wakiacha msala wa kumuhudumia mchezaji yule kwa uongozi ambao nao unakuwa hauna fungu la kummudu, hivyo kupelekea madeni ya malimbikizo ya mishahara. Tatizo ambalo limekuwepo miaka nenda rudi ndani ya vilabu hivi.


Halafu kwa Simba bado nashindwa kuelewa wapi walipopeleka fedha nyingi ambazo walizipata kutokana na mauzo ya wachezaji kama Mbwana Samatta, Musa Mgosi, na Patrick Ochan,moja ya sababu ambazo Kelvin Yondan kuwa na mgogoro nao ni kutokana kudai kwamba Simba walimkopa fedha za usajili wakati akisaini mkataba mpya. Haya ni matokeo ya timu hizi kujiendekeza na kutokuwa na mipango endelevu ya kuweza kujitegemea zenyewe bila kusubiri kutembeza bakuli kwa watu wanaojiita wadau ambao siku zote wamekuwa ndio wanatumia fedha zao kuvuruga amani kwenye vilabu hivi pale wanapoona interest zao zinaingiliwa.


UTEGEMEZI WA MAPATO YA MILANGONI
Ukiachana mkataba walionao Simba na Yanga kutoka TBL, Vilabu hivi siku zote vimekuwa tegemezi kwa mapato yanayotokana na get collections kuweza kugharamia mambo mbalimbali katika kuziendesha timu hizi mbili. Lakini siku hizi kumekuwepo na utaratibu wa kutoa bonasi kwa wachezaji kila mechi ambazo zinakuwa na matokeo ya sare au kushinda. Pale timu inaposhinda basi asilimia kubwa ya mapato ya milangoni yanaashia kwenda kwa wachezaji, hivyo kile kidogo kinachobakia hakitoshi kuweza kuendesha kwa kugharamia vitu vingine kama vile kulipa mishahara. Japokuwa wanapata fedha fulani kwa mdhamini wao TBL kila mwisho wa mwezi lakini fedha hizo hazitoshelezi kwa sababu Yanga na Simba vinalipa mishahara mikubwa kuliko kile wanachoingiza. Mwisho wa siku ndio unakuta wachezaji wanakopwa mishahara yao mpaka miezi mitano na kuendelea huku wakiambulia posho za mapato ya getini ikiwa timu inashinda au kutoa sare.


Kwa mfumo huu soka letu litaendelea kupata wakati kuendelea mbele. Simba na Yanga badilikeni, viongozi acheni kuvitumia vilabu kwa manufaa yenu binafsi.

3 comments:

  1. makala yako kaka shafii imetulia. ila nataka nitumie sehemu hii kukukosoa kidogo kama mwanafunzi wako KTK uchambuzi wa soka la kibongo.
    siku zote kocha ndie anaependekeza jina la mchezaji anaemuhitaji kwa ajili ya kumtumia. ni wazi kwamba mchezaji atakae pendekezwa na kocha huyo ni kwamba amekidhi vigezo vya kocha. na kamwe kocha huyo haja kurupuka ispokuwa amemsoma mchezaji huyo kwa mechi zaidi ya kumi ili kuthibitisha uwezo wake na si kwa mechi moja ama mbili. lazima utambu kaka shafii kuwa ligi yetu sio PUBLIC, kwa maana ni vigumu kuziona timu zote zinapocheza zaidi ya kuona ile unayocheza nayo wakati huo. ni dhahiri kaka kuwa kocha yoyote wakigeni hawezi akachagua kikosi bora zaidi ya wale aliowaona yeye kwa mechi mbili tatu vingenevyo kocha huyo amekaa kwa mda mrefu. nadhani hutakataa nikisema kwamba yule mseribia wa yanga au wa simba hawezi akaiyona mechi kama toto na kagera. moro na jkt ruvu n.k. timu hizo ataziona wakati akicheza nazo. unadhani kwa staili hii hata makocha hawa nje ya nchi wakipewa mamlaka ya kusajili timu watapata wachezaji wanaokidhi vigezo?
    kamwe kaka usifananishe taratibu za usajiliza ulaya na hili soka mchafu koge( soka la bongo) kule ulaya kocha wa baca, madrid, inrter, juve, bayan, n.k wanaweza kusajili mchezaji nje ya mipaka ya nchi zao kwa sababu soka lao ni PUBLIC linaonekana sehemu mbali mbali hivyo makocha wanauwezo wa kumfatilia mchezaji mwanzo wa ligi mpaka mwisho wake na akathibitisha uwezo wake. lakini sisi hatuwezi kumsajili mcheza hata wa kenya kwa ubaora wake zaidi ya kumuona mechi mbili tatu kenye kagame, tusker, na chalenge. hata kama mchezaji huyo aling'ara kwa vimechi viwili vitatu bado haitoshi kumuamini moja kwa moja na kumpa mkataba mrefu wa miaka miwili. itakumbukwa kwamba hata makocha wanakabithiwa taifa star hawasajili kwa kutazama kiwango endelevu bali wanaangalia kiwango cha mpito cha mchezaji kwa mfano maximo alimsajili MWAIKIMBA, KIM PSN amemsajili john boko, lakini cheche zao hazikuonekana. hhivyo kaka kwa soka la bongo hata kocha akipewa fursa ya kupendekeza mchezaji hawezi aka pata the best labda awe amekaa tz kwa zaidi ya misimu mitano ya ligi.
    kwa upande wa uongozi wa vilabu vyetu tukubali tukatae lazima timu zikubali kuendesha kikampuni hilo ndio suluhisho. vinginevyo wezi watazidi kuvifilisi hivi vilabu. kwa mfano mwenyeketi aliyejiuzulu NCHUNGA amelalamikia sana ukata wa club na kushindwa kuwalipa wachezaji na makocha stahiki zao. kimsikiliza kwa harakaharaka utasema ukosahihi lakini ukitazama nyenendo zake na maneno yake utagundua kuwa nchunga, na viongozi wetu wa simba na yanga ni tatizo. hivi kweli seheemu ambayo huna maslahi nayo unaing'ania ya nin? kwa nini alikuwa mgumu kujiuzulu wakati anajua kuwa yanga ilikuwa na matatizo makubwa ya kiuchumi yaliyosababisha timu kufanya vibaya? hivi hakumuaona mwenzake MOSHA alipo jiuzulu makamo mwenyekiti na akasema wazi kwamba alikuwa akitumia hata pesa zake mfukoni kuipa yanga lakini bado baadhi ya wanachama walimpinga hivyo akaamua kujiweka kando. je ilichukuwa mda gani wanachama walikua hawakauki kwenda kwa MOSHA kumbeleza arudi? hii ilidhihirisha kuwa yeye aliisaidia yanga bila kupata chochote. mfano mwengine MANJI alikwaruzana na wazee na wakamtaka akaepembeni awaachie club yao, na MANJI alifanya hivyo. je ni mda gani ulipita wazee walirudi tena kumbembeleza MANJI arudi yanga? hii ilidhihirisha msaada wao kwa yanga. SASA kwa nini ndugu yangu nchunga alikuwa mgumu kuachia ngazi ilihali alikuwa anasema anajua kwamba timu ilikuwa ngumu kuiendesha kutokana na ukata? LAZIMA UKUBALI KAKA shaffih kuwa njaa ni tatizo kwa viongozi wa vilabu vyetu vya simba na yanga. na kukataa kwao vilabu hivi kuendeshwa kikampuni ni tatizo zaidi kwa vilabu vyetu....... NAWASILISHA

    ReplyDelete
  2. Unajikosha hamna coverage ingine, si wafafanulie we ni Yanga maana hawakujui kuwa mwenzao!

    ReplyDelete
  3. W
    MIMI NAONA NA WEWE HAPO JUU UNAKOSEA. MIMI NIKO HUKU ULAYA KTK MFUMO WA HUKU TIMU ZINAKUWA NA MASCOUT KAMA WATATU MPKA WANNE AAMBAO WANAKUWA WAMEAJIRIWA NA WENGINE WANAKUWA WANALIPWA KWA ASILIMIA KAMA ATAWEZA KUMSCOUT MCHEZAJI NA AKASAJILIWA NA CLUB. HAWA KAZI YAO NI KUTAFUTA VIPAJI NA HUWA WANASAFIRI SEHEMU MBLIMBALI DUNIANI NA WAMEKUWA KITAALAM ZAIDI KWA KUWA NA VIFAA KAMA VIDEO CAMERA N.K.AKIWA NA UHAKIKA NA MCHEZAJI ANATOA TAARIFA KWA KAMATI YA UFUNDI KWA VIELELEZO VYOTE, KOCHA YEYE KAZI YAKE NI KUANGALIA SEHEMU GANI ANAMAPUNGUFU NA KUTOA TAARIFA KWA KAMATI YA UFUNDI, NA PIA ANAWEZA AKATOA MAPENDEKEZO KAMA NA YEYE AMEMUONA MCHEZAJI ANAYEFAA KATIKA TIMU ANAZOKUTANA NAZO. SCOUT AKILETA TAARIFA NDIPO KAMATI YA UFUNDI INAMTAARIFU KOCHA NA KOCHA KWA KUANGALIA CV YA MCHEZAJI NA VIELELEZO VINGINE ANAWEZA AKAOMBA AJE KUFANYA MAJARIBIO AMA ANAWEZA KWENDA KUMUANGALIA AKICHEZA. SASA KWA TIMU ZETU SIMBA NA YANGA ZINAWEZA KUWA NA MASCOUT KWANI HAKUNA SEHEMU MBALI HAPA DUNIANI. MIMI NAMUELEWA SHAFFIH. KUMBUKA HUKU ULAYA HAKUNA GATE COLLECTION ETI WAKAPEWA WACHEZAJI ASILIMIA KITU HICHO HAKUNA. GATE COLLECTION NI PESA YA CLUB KUJIENDESHA, MPIRA NI KAZI KAMA KAZI NYINGINE BORESHA MISHAHARA YA WACHEZAJI TOA HIYO CATE COLLECTION TAFUTENI MIRADI KAMA KUUZA JEZI TAFUTENI WADHAMINI NA MAKAMPUNI AMBAYO NDIO KAZI YA VIONGOZI NA SIO KUSAJIRI TIMU. NINI KAZI YA TECHNICAL BENCH? KAMA KIONGOZI ATASAJILI. TECHNICAL BENCH KIBONGOBONGO NI KUTAFUTA UCHAWI

    ReplyDelete