Search This Blog

Friday, June 22, 2012

KENNETH ASAMOAH ATEMWA YANGA - KULIPWA FIDIA

Hatimaye mshambuliaji wa Yanga kutoka Ghana Kenneth Asamoah ametemwa na klabu hiyo baada ya kuitumikia kwa takribani msimu mmoja tu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Yanga, Asamoah amefikia makubaliano na Yanga kwa kulipwa fidia ya kuvunjiwa mkataba wake aliousaini msimu uliopita.

Kenneth Asamoah anaondoka Yanga huku akiwaachia wapenzi wa klabu hiyo kumbukumbu ya goli zuri la kichwa alilowafunga Simba kwenye fainali ya kombe la Kagame mwaka jana kwenye uwanja wa Taifa.

4 comments:

  1. Sasa ni dhahiri Meddy Kagere a.k.a Magoli yuko njiani kutua Jangwani,safi sana viongozi wa Yanga

    ReplyDelete
  2. sasa yanga mmeamua. hivyo ndivyo inavyo takiwa. mchezaji kama hakuonesha kiwaango kuachwa nilazima. msiogope kuvunja mikataba kwa wazembe kama hao ilimradi muwalipe stahiki zao. YANGA OYYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.SIMBA WAJIANDAE GOLI SITA ZINAKUJA. SISI tunawatema akina mwape hao wanasajili kina mwape wengine kutoka kongo. TUMEJIFUNZA wachezaji wazuri wapo hapahapa bongo ukitoka nje labda rwanda au uganda. lakini mchezaji atoke gana aje bongo au aache TP MAZEMBE kule kongo AJE BONGO. ujue HILO NI GARASA.

    ReplyDelete
  3. Pumbafuuu, si huyu huyu asamoah mlimbeba pale DIA na kumkejeli sana Rage, sasa mnamuona kinyesi sio, wachezaji wako humu humu bongo sio, ndo maana mkaona Yondani mumchukue? mjue mmechemka, Yanga hamuwezi kupandisha viwango ila kushusha kila siku sisi Simba ndo wanaume zenu wa kutengeneza wachezaji na nyie mje tu kubeba, angalia Makasi atakuwa Jembe si muda mpaka mtamtamani km kawaida yenu, unasema Yanu ni garasa? ngoja uone kazi yake ile mashine kuliko hata Nyonzima kwa taarifa yako ukijumlisha na Kinje ndo inakuwa balaa, Nani wa kutufunga 6 Yanga...............? hilo ondoa mkuu, mshakula zile 5 zinawatosha.

    ReplyDelete
  4. Wachezaji wazuri na klabu na migogoro wa uroho hakuna mafanikio hata mmsajiri drogba aje kuwa mchezaji wenu jangwani pole mtatukuta kagame tuwanyowe paza zenu

    ReplyDelete