Search This Blog

Saturday, May 5, 2012

PAPISS DEMBA CISSE: KLABU TANO KUBWA BARANI ULAYA AMBAZO ZINAJUTA KUTOMSAJILI MSENEGALI HUYU

Kipindi cha kiangazi mwaka 2011 wakati Papiss Cisse akiwa anaichezea SC Freiburg - akiwa amefunga magoli 22 katika mechi 32 za Bundesliga - hakuna klabu iliyokuwa tayari kumsajili.

Hiyo ni kwasababu alikuwa anauzwa kwa £14 million, ada ambayo hakuna kocha au bodi ya wakurugenzi ilikuwa ipo radhi kulipa, especially kwa mchezaji ambaye hakuwa na hata na uzoefu mkubwa katika mechi ya level ya juu - pamoja na kuwa mchezaji wa kulipwa kwa takribani miaka 7.

Timu nyingi zilisemekana kuvutiwa nae - na chache zikatuma maskauti -lakini hakuna klabu iliweza kutuma ofa, na dirisha la usajili la kiangazi likafungwa huku kukiwa hakuna dili yoyote iliwasili Ujerumani kwa ajili yake.

Mwezi January dirisha la usajili likafunguliwa - na klabu zikaendelea kumtamani, japokuwa term hii alikuwa kafunga mabao 9 tu katika michezo 17.

Ada ikashuka mpaka £10million, na timu chachezikaonyesha kuvutika lakini ilikuwa ni Newcastle United ambao waliinyakua almasi toka mchangani.

Kocha Alan Pardew akiweka imani kubwa kwa Cisse na kumsaini kwa mkataba wa miaka mitano na nusu..

Toon walikwa ndio klabu pekee ambayo walitumia naasi na kumsaini mshambuliaji huyo na kumpa nafasi ya kucheza kwenye ligi ya level ya juu.

Michezo 12 ya Premier league baada ya kusajiliwa kijana wa miaka 26 kutoka Senegal kiukweli ameanza kulipa  fadhila, akifunga magoli muhimu 13 - likiwemo moja ya magoli bora kabisa kuwahi kutkea kwenye soka dhidi ya Chelsea.

Hizi ni klabu tano  - ambao ukizingalia kwa sasa - kwa hakika watajuta kutolipa £10million na kumsaini Papiss Cisse walipokuwa na nafasi ya kufanya hivyo.


BLACKBURN ROVERS
Ndio, Blackburn Rovers wangeweza kumsaini Papiss Cisse. Hivi ndivyo wakala wa mchezaji huyo alivyosema mwezi June 2011: "Blackburn waliamuangalia karibia mara 10 msimu uliopita na nilionana na skauti wao. Lakini hatukusikia chochote kutoka kwao."

Taarifa zinasema walituma ofa iliyokataliwa ya £6 million kwa Cisse, na walitakiwa kuongeza mpaka £12 million, lakini hawakuwahi kufanya hivyo.

Yukubu Aiyegbeni ndio ni mshambuliaji mzuri kwa Blackburn - ukifikiria amefunga mabao 16 katika mechi 29 msimu huu - lakini ikiwa Rovers wangekuwa na world class striker kama Cisse,  katika timu yao, then nafikiri nafasi ya 19 waliopo katika premier league isingekuwa mahala walipo sasa.


SUNDERLAND
Mashabiki wa Newcastle watachukia kufikiri, lakini Papiss Cisse angeweza kujiunga Sunderland mwezi January.

Aliripotiwa kuwa amevutiwa na interest ya Sunderland, huku ripoti nyingine zikisema kwamba manager Martin O'Neill angejaribu kumsaini mshambuliaji huyo.

Lakini chelewa chelewa ikawagharimu Sunderland, baada ya Newcastle ambao ni mahasimu wao wakubwa wakathibitisha kumsaini Cisse.

Ni kitu ambacho kinaweza kuwaandama Black Cats kwa misimu mingi ijayo ikitazamwa impact aliyonayo Cisse kwa wapinzani wao.


TOTTENHAM HOTSPUR
Spurs nao walikuwa wametajwa katika mbio za kutaka saini ya Cisse, na ilikuwa ikifikiriwa kwamba wangetuma ofa yao mwezi January 2012.

Lakini Spurs walisubiri kwa muda mrefu, wakampoteza kwa Newcastle, na wakafanikiwa kumsaini Louis Saha kutoka Everton.

Walifuata uafadhali badala ya ubora - wakagoma kutoa hela na kumsaini Sha bure - na hili linaweza likawa limewagharimu kuchukua ubingwa - na hata inaweza ikawa nafasi ya kushiriki UEFA Chmpions league.


FULHAM
Fulham ilikuwa ni klabu nyingine ya premier league ambayo ilipoteza nafasi ya kumsaini mshambuliaji wa daraja la juu na mtambo wa magoli Papiss Cisse.

Mwezi wa nane 2011, baada ya Cisse kusema njooni mnisajili kwa timu yoyote yenye pesa nchini England kumnunua, oliripotiwa kwamba the Cottagers walikuwa wapo tayari kutoa £14 million zilizokuwa zikitakiwa na Freiburg.

Kama ilivyo kwa wengine West Londoners nao wakazubaa zubaa na walkapoteza nafasi ya kumsajili msenegal huyo ambaye sasa ni sumu ya mabeki nchini Uingereza.

Bryan Ruiz alisajiliwa kutoka FC Twente kwa £10.6 million - ambazo zilikuwa nyingi zaidi ya Newcastle walizolipa kwa ajili ya Cisse.

Katika michezo 27 na Fulahm, Ruiz amefunga mabao mawili tu. Kwa pesa kidogo wangeweza kumsaini mtambo wa magoli. Watajuta.


JUVENTUS
Wanaweza wakawa kwenye nafasi nzuri ya kuchuku a ubingwa ambao pia wanaweza wakaupoteza kwa AC Milan, lakini kwa timu ambayo inahitaji sana mshambuliaji,  ni kesi ya je ingekuwaje kama Juve wangemsajili Papiss Cisse.

Kibibi Kizee cha Turin waliripotiwa na vyombo vya habari vya Italia kwamba walikuwa radhi kulipa pesa waliyotaka Freiburg. Lakini badala ya Cisse wakaamua mwishowe kumsaini Alessandro Matri, ambaye katika mechi 30 amafunga mabao 10 - na kama kwa hesabu za haraka haraka na kufikirika Cisse angeweza kuwa ametupia magoli mabao 33 katika idadi hiyo ya mechi.

Cisse amegeuka na kuwa investmen nzuri, na kama Juventus wangemsajili na angekuwa kwenye kiwango hiki ama kwa hakika sasa hivi wangekuwa wameshatangaza ubingwa mbele ya AC Milan.

1 comment:

  1. Cisse jembe tena hatari mno, mimi nafikiri hawa wenzetu wazungu wakati mwingine wanaleta dharau ndio maana unaona walikuwa wanajivutavuta ila kama angekuwa mwenzao wakiona dalili tu watu wanalipa pesa ngoja jamaa alipe fadhila huko Newcastle hao waliokuwa wanaleta nyodo wataipata habari yao,
    Shaffih nasikia Rashid Yekini moja kati ya malegendary wa hatari katika soka toka Nigeria amefariki dunia bwana.R.I.P Rashid Yekini.
    Mdau
    Mike.

    ReplyDelete