Search This Blog

Saturday, May 5, 2012

Shujaa wa soka Nigeria Yekini afariki

Rashid Yekini afariki dunia
Rashid Yekini

Mcheza kandanda bora mara mbili barani Afrika, Rashidi Yekini amefariki dunia.
Yekini alizaliwa katika jimbo la Kaduna mwaka 1963. Baada ya kuanza kucheza kandanda ya kulipwa kwenye ligi nchini Nigeria, alikwenda Ivory Coast kuichezea klabu ya Africa Sports. Baada ya hapo alitimkia Ureno ambako alikuwa mfungaji mabao hodari katika ligi ya daraja la kwanza ya Ureno ambapo msimu wa 1993–94 alikuwa amepachika mabao 34 katika mechi 32 alizocheza.
Kupanda kwa kiwango chake cha usakataji kabumbu akiichezea timu ya taifa ya Nigeria msimu huo ambapo Nigeria ilishiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya Kombe la Dunia na baadae kufuatiwa na Kombe la Mataifa ya Afrika, alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika mwaka 1993, akiwa mchezaji wa kwanza wa Nigeria kupata tuzo hiyo.
Rashid Yekini, ambaye alikuwa ametalikiana na mkewe tangu mwaka 1994 alikuwa akiishi maisha ya tabu na wapangaji wengine wachahe katika nyumba yake mjini Ibadan, jimbo la Oyo ambapo iliarifiwa mara chache sana alikuwa akitembelewa na wageni.
Yekini amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 49. Ameacha watoto wawili. Anazikwa siku ya Jumamosi kwa mujibu wa taratibu za dini ya Kiislamu huko Irah, jimbo la Kwara.

No comments:

Post a Comment