Search This Blog

Friday, May 25, 2012

FAMILIA YA MAFISANGO YAOMBA MSAADA SIMBA NA AZAM


FAMILIA ya aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa Simba na timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’, Patrick Mutesa Mafisango, imeomba msaada kutoka kwa klabu ambazo marehemu alizitumikia miaka ya hivi karibuni.


Marehemu Mafisango, kabla ya kutua Simba na hivi karibuni kurejeshwa Amavubi ambako pia aliwahi kuwa nahodha, alikipiga kwa wana Lambalamba, Azam FC.

Akizungumza katika mahojiano nA Clouds TV hivi karibuni, nyota wa zamani wa Simba, ambaye anakipiga timu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC), Mussa Hassan Mgosi, alisema kifo cha mchezaji huyo ni pigo kwa familia yake na hasa watoto wake watatu aliowaacha.

Mgosi alisema kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu nchini Congo na jinsi ambavyo familia hiyo ilikuwa ikimtegemea marehemu kwa kuwatumia fedha ili waweze kujikimu na hali ngumu ya maisha, huu ni muda muafaka kwa Simba, Azam na Amavubi kutoa sapoti, walau familia hiyo iweze kujikimu.

Aidha mbali na timu hizo, Mgosi aliwaomba wachezaji kutoka Simba, Azam na wadau mbalimbali, kujichanga na kila mtu kutoa kile alichonacho ili waweze kuliokoa jahazi ambalo mpiganaji mwenzao ameliacha.

Marehemu Mafisango, alifariki usiku wa kuamkia Mei 17 kwa ajali ya gari katika eneo la Veta Chang’ombe jijini Dar es Salaam na kuzikwa mwishoni mwa wiki iliyopita, katika makaburi ya Kinkole nje kidogo ya jiji la Kinshasa. Marehemu ameacha wake watatu na watoto watatu.

2 comments:

  1. Kiongozi,
    Binafsi jinsi hizi Club 2 lkn zaidizaidi Simba walivyouchukulia huu msiba wa Mshikaji imenishangaza sana,pamoja na kushindwa kutoa mwakilishi anayeeleweka kutoka ngazi ya juu ya uongozi kuambatana na mwili wa Marehemu katika safari yake ya mwisho humu Duniani hata rambirambi hakuna....jamani embu waone aibu,ile familia imepoteza mwelekeo kabisa kama wameshindwa kumuelewa Mgosi hivi hata picha wanashindwa kuangalia,hawaoni (katika picha) jinsi wafiwa walivyopoteza matumaini,sitaki kuamini siku chache tu tokea afariki Simba leo wamesahau kabisa makubwa aliyowafanyia tena mengine kwa juhudi zake binafsi,hivi yale ma'elfu 10,10 waliyokuwa wanamtunza baada ya wonders zake katika game wanaona tabu gani kuzikusanya na kuwapelekea wafiwa angalau ziwasimamie kwa kipindi hiki wakati wakitafuta namna nyingine ya kuishi?
    Hizi si laana hizi wanazozitafuta.....

    ReplyDelete


  2. Have a look at my web site; pit 38 wzór

    ReplyDelete