Search This Blog

Friday, May 25, 2012

TFF: HATUTOMLIPA HATA SENTI MOJA JAN POULSEN


SHIRIKISHO la Soka Tanzania(TFF) limeweka wazi kwamba aliyekuwa kocha wa timu ya taifa(Taifa Stars)Mdenmark Jan Poulsen hatalipwa mishahara yake ya miezi mitatu iliyosalia katika mkataba wake.

Msimamo huo wa TFF umekuja baada ya  gazeti la Mwananchi wiki iliyopita kumkariri Poulsen akililalamikia shirikisho hilo lwa kutolipwa mshahara wake wa mwezi mmoja,sambamba na fidia inayotokana na kuvunjwa kwa mkataba wake.
Hivi karibuni TFF ilisitisha huduma ya Poulsen kwa Taifa Stars na badala yake ikamtangaza aliyekuwa kocha wa timu za taifa za vijana, Kim Poulsen kuchukua jukumu hilo.

Akizungumza na Mwananchi, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa hatua ya kutomlipa Poulsen mishahara ya miezi mitatu inatokana ukweli kwamba kocha huyo hatakuwa na kazi ya kufanya katika kipindi hicho cha miezi mitatu ya mkataba wake kilichosalia hadi Julai 30.

"Kwanza kabisa ieweweke kwamba serikali ndiyo iliyokuwa inamlipa  Poulsen mshahara baada ya kuingia naye mkataba na sio TFF."Katika utaratibu wa kawaida wa serikali tunaoufahamu awezi kulipwa mshahara wa bure wakati hajafanya kazi yoyote,huo ndio ukwli wenyewe,"alisema Wambura

Akifafanua zaidi, Wambura alisema TFF iliamua kusitisha huduma za Poulsen licha ya kwamba mkataba wake unaendelea kuwa hai kwa lengo la kuta nafasi kwa kocha mpya kupanga mipango ya muda mrefu.

"Kila baada ya muda fulani kocha anatakiwa awasilishe ripoti ya timu yake,sasa utapataje ripoti sahihi wakati kesho kutwa mkataba wake unamalizika.

"Pia niweke vizuri hapo,TFF haikuvunja mkataba wa Poulsen bado upo na utamalizika Julai 30 tulichokifanya ni kuzungumza nae na kukubaliana kwamba hakutaongeza mkataba hivyo tunatafuta kocha mwingine,"alisema.

Wambura aliongeza kuwa,licha ya kibarua cha kocha huyo cha kuinoa Taifa Stars kusitishwa,bado TFF itaendelea kuwa nae katika mkataba mwingine unaohusiana na ukufunzi wa makocha nchini.

"Poulsen pia alikuwa na kazi nyingine ya ukufunzi wa makocha hata hapa ametuaga anakwenda kwao kuhudhuria harusi ya mtoto wake akirudi ataendelea,"alisema Wambura

Kwa  upande mwingine kusitishwa kwa kibarua cha Poulsen kunahusishwa  na shinikizo la wadau wa soka waliotaka mabadiliko katika benchi la ufundi kufuatia Taifa Stars  kuporomoka mfululizo kwa takribani miezi saba kwenye viwango vya ubora vya Shiriki

4 comments:

  1. TFF kama club za simba na yanga,sheria za kazi na ajira zipo wazi kabisa,TFF waache ubabaishaji wamlipe pesa zake na gharama za mkataba,waache uhuni

    ReplyDelete
  2. Jamani nchi hii kuna watu kweli wa kuongoza kitu kwa kufuata sheria?, TFF ndio iliosema kocha ukae pembeni kwa kuwa kiwango cha timu hakiongezeki zaidi ya kushuka na pia hatutaongeza mkataba wako. Sasa katika hali ya kawaida sio kuuvua uhalali mkataba wake?. Hicho kinaitwa mutual agreement. Je, kwenye mutual agreement si kuna fidia fulani inatakiwa kocha apewe ili akubali kuondoka?. Vinginevyo atasema mmevunja mkataba so mmulipe haki zake zote. kuweni wazi kama kuna fidia mlimpa ili tuwaelewe acheni kuongea kama mnaongoza mandina. Mfano Mourinho aliondoka Chelsea kwa Mutual agreement. sasa mbona nyie hamueleweki?, eti hatuongezi mkataba wakati haujaisha then?????, kwa nn usimlipe chochote?

    ReplyDelete
  3. Mambo ya ushwahilini hayo. Wewe utakataaje kumlipa mtu kienyeji kinyeji tu. Kwani si umesema mlikaa makakubaliana? Aiibuuuuuuu!!!

    ReplyDelete
  4. TFF acheni utapeli! kama mkataba unaisha July 30 ni haki yake kisheria kulipwa mpaka mda huo,wakati mwingine mtafakari cha kuongea sio mnatoa tu matamko,mjue kile mnachoongea ndio umma unatambua uwezo wenu wa fikra na kwenye majukumu

    ReplyDelete