Search This Blog

Thursday, May 10, 2012

BAADA YA MASAA MANNE BARABARANI SIMBA YAFIKA MJI WA SHANDY KWA TAABU: WENYEJI WAWAKIMBIA - HAWAJALA KITU CHOCHOTE KWA MASAA TAKRIBANI SITA SASA

Hatimaye baada ya masaa manne ya kusafiri kutoka Khartoom mpaka Shandy wawikilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ya soka Simba SC imefika mjini Shandy salama kabisa.

Lakini katika hali ya kushangaza wenyeji wao timu Al Ahly Shady wamepotea na kuwaacha wageni wao Simba katika hali tata - kwa mujibu wa mchezaji Emmanuel Okwi wamefikia sehemu mbaya na tangu wamefika takribani masaa sita yaliyopita hawajitia kitu chochote mdomoni. "Bwana huku tumefika lakini kwa shida sana, tunashukuru mungu tumefika salama ila tangu tumefika hapa hatujatia kitu chochote mdomoni na wenyeji wetu hawaonekani. Ila tunawaomba wanasimba na watanzania kwa ujumla waendele kutakia kheri na tunawahidi hizi hila za wasudani hazitowaepusha na kipigo siku ya mechi." - Emmanuel Okwi.

6 comments:

  1. Msianze visingizio hy hamkuyajua?askari hachagui pori,kazeni bwana

    ReplyDelete
  2. tuko pmj na simba sc pmj na fitna wanazowanya wasudan naamin tutashinda inshallah na kusonga mbele.... its me kwanja jr from fc boom ilala

    ReplyDelete
  3. Wewe unayesema ni visingizio umelala, wala hujui linaloendelea. Huna tofauti na yule mkereketwa wa Yanga anayelaumu TFF kwa kile kichapo cha kwenye majuzi, anawalaumu pia waandishi wa habari, ... hebu ntoleeee hapa!!!

    Huamini hayo kwa kuwa u mpwefu, unasikia tu wala hujawahi kushuhudia laiv! Kwa taarifa yako hata Algeria mambo hayakuwa rahisi. Kulikuwa na kila aina ya vitimbwi ikiwa ni pamoja na kutelekezwa airport kwa zaidi ya masaa matatu, kutosafirishwa kwenda Setif kwa taratibu za CAF, waandishi wa habari kunyang'anywa vifaa vya kazi (cameras etc.), hujuma katika hoteli waliyofikia kule Bordj El Kifan (ilibidi taratibu binafsi za misosi ziandaliwe), usafiri wenye lengo la kuichosha timu etc.

    Pale Setif, ilibidi timu iwasubiri wenyeji wamalize mazoezi ili Simba iweze kuanza kupasha misuli, kwa kawaida timu ngeni hupewa uwanja bila vikwazo siku moja kabla ya mchezo. Haikuwa hivyo. Kule Hotel Zidane purukushani za hapa na pale hazikuisha dhidi ya wachezaji na washabiki wachache watanzania. Kuna kipindi washabiki walivamiwa na kunyang'anywa vuvuzela, kuibiwa simu etc. etc.

    Miaka karibu miwili iliyopita, Taifa Stars ilikumbana na vimbwanga vinavyofanana na hivyo. Niliona kwa macho yangu mwenyewe, siandiki 'kwa kudhania' kama wewe eddo unavyofanya. Uwe 'feaa' ndugu, Simba wanakabiliwa na mtihani mkuu.

    ReplyDelete
  4. Eti mnajifanya kushangaa kusafiri masaa manne,kwani nyie kwenu Frolida usa?twawajua vizuri nyie wote kwenu kwenda ni kwatrekta au miguu zaidi yamasaa sita,leo mnajifanya kudeka eti tumesafiri kwabasi masaa manne,nyambaff.

    ReplyDelete
  5. WAPENZI WA SIMBA WOTE MSIWE NA SHAKA NI KWA MARA YA KWANZA TUTASHIDA UGENINI SIMBA 2-0

    ReplyDelete
  6. MSIKATE TAMAA WEKUNDU WA MSIMBAZI TUKO PAMOJA.KILA LA KHERY.

    ReplyDelete