Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), imesitisha udhamini wake kwa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ulioanza mwaka 2006 kutokana na dau la kuidhamini timu hiyo kupandishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Stori zimeamplfy kwamba SBL iliyoanza kuidhamini Taifa Stars kwa dau la Sh. Milioni 700, imetakiwa na TFF kutoa Sh. Bilioni 3.6 kwa mwaka kuidhamini.
Ofisa mmoja wa TFF, ambaye hakutaka kutajwa jina aliiambia bongostaz jana kwamba pamoja na hayo, mazungumzo bado yanaendelea kati ya pande hizo mbili japo inasemekana pia shirikisho limeahidiwa udhamini mnono kutoka kampuni nyingine kubwa ya bia nchini.
“Lakini kwa kuzingatia pale ambapo SBL wameitoa Taifa Stars, waliichukua haina mdhamini na hakuna mtu au kampuni iliyokuwa tayari kuidhamini, wamefanya mambo mengi kwa manufaa ya soka hii, kwa kweli hata mimi ningependa SBL iendelee kudhamini timu hii,” alisema Ofisa huyo.
TFF iliipandishia dau la udhamini SBL kutoka Milioni 700 hadi 800, baadaye 900 na mwaka jana ilikuwa n Sh Bilioni 1.2 ambapo sasa TFF inataka Bilioni 3.6 kwa mwaka na kwa sababu mkataba wa udhamini baina ya pande hizo mbili uliisha tangu Desemba, Taifa Stars haina mdhamini kwa sasa.
Taarifa kutoka TFF na SBL ni kwamba kuna mazungumzo yanaendelea kati ya pande mbili kuona kama mkataba mpya utasaini wa ama vipi.
No comments:
Post a Comment